Wema Sepetu akichekelea
Mama mzazi wa staa wa Bongo Wema Sepetu
SIJUI ni hasira au nini! Mama mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu ‘Mama Wema’ amemshika uchawi mpenzi wa bintiye, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akilaani vikali kitendo cha kumrudia mwanaye akidai lengo lake ni kumharibia maisha, Ijumaa Wikienda lina mkasa kamili mkononi.
Diamond kwenye moja ya pozi zake
Mama Wema alitoa hisia zake hizo juzi jijini Dar es Salaam alipoongea kwa simu na paparazi wetu huku maneno yake yakiwekwa kwenye kumbukumbu ya kinasa sauti cha Global Publishers.
ALIANZAJE?
Mwanamke huyo mwenye msimamo uliopitiliza kuhusu bintiye Wema, aliwasiliana na paparazi wetu akisema siku hiyo anataka kutoa dukuduku lake kuhusu Diamond ambaye pia ni staa wa Bongo Fleva.
Mama Wema alisema taarifa alizonazo kuhusu staa huyo ni kwamba, juzikati alikwenda kwa mganga f’lani na kuzika kondoo watatu ili Wema aharibikiwe maisha.
“Mimi nimekerwa sana na huyo Diamond wenu. Najua hajamrudia Wema kwa mapenzi, amemrudia ili apate nafasi ya kumharibia maisha. Ni kijana hatari sana.
“Nina taarifa kutoka kwa watu wa karibu naye kwamba alikwenda kwa mganga akazika kondoo watatu ili mwanangu aharibikiwe.
“Simpendi na sitaki hata kumwona. Hana nia nzuri na mwanangu, najua. Kwanza mama Diamond (Sanura Kasim) hampendi Wema, anampenda Penny, nampongeza sana kwa uamuzi huo,” alisema mwanamke huyo.
AMSHANGAA DIAMOND KULALIA KITANDA CHA KIGOGO WA IKULU
Mama Wema ambaye anasifika kwa ubabe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa amesikia Diamond sasa analala na kula kwa Wema. Akatolea tamko kitendo hicho.
“Kama angekuwa mwanaume kweli ana pesa zake angekubali vipi kulala kwenye kitanda alichonunua mwanaume mwenzake (Clement)?
Wema.
“Hiyo ni akili kweli? Vitu anunue mwanaume mwenzako halafu wewe uje kutumia bila haya. Halafu nimesoma kwenye gazeti moja (Amani) eti atamnunulia Wema vitu vyote alivyonyang’anywa na Clement, mimi nasema hawezi kumnunulia kamwe, anamdanganya tu,” alisema mama Wema.
ANACHOTAMANI
Mama Wema hakuacha kutoa donge lililokaa juu ya moyo wake, alisema:
“Nimeshamaliza arobaini ya mume wangu (Mzee Isaac Sepetu). Natamani siku moja nimfuate Diamond popote alipo nikamtandike makofi mpaka ashike adabu yake mwana…(tusi).”
AMPA TAHADHARI YA KUMKATA NA PANGA
Paparazi wetu alimpomuuliza mama Wema kama yupo tayari kumkaribisha Diamond nyumbani kwake ili wayaongee na kuwekana sawa na abariki uhusiano wao wa kimapenzi, alikuja juu.
“Aje wapi? Aje aongee na nani? Asije akajaribu kuja nyumbani kwangu, haki ya Mungu tena nitamkata na panga, hivi yule…(tusi) ananijua hanijui?”
ASEMA HAKUNA MZAZI YEYOTE ANAYEKUBALI UHUSIANO WA DIAMOND NA MTOTO WAKE WA KIKE
Mama huyo alizidi kuweka wazi kuwa hakuna mzazi yeyote Tanzania mwenye uchungu na mwanaye anayeweza kuruhusu uhusiano wa Diamond na mtoto wake wa kike.
“Nataka kukwambia kwamba hakuna mzazi yeyote hapa Tanzania anayeweza kukubali ujinga anaoufanya Diamond kwa mwanaye wa kike. Ni mtu gani ambaye hapendi kabisa kuwa mtulivu zaidi ya kuwachafua wasichana? Mimi naumizwa sana na yeye,” alisema mama huyo huku akisisitiza maneno yake yaandikwe gazetini.
WEMA YAKIMSHINDA ARUDI NYUMBANI
Bi. Mariam alizidi kutoa ya moyoni mwake na kusema kuwa inawezekana Diamond anafanya hivyo akijua kuwa Wema hana pa kwenda akishamuacha mweupe baada ya kumharibia uhusiano wake na Clement.
“Najua Diamond anaamini akishamchezea Wema na kumwacha atakuwa akitangatanga, lakini akumbuke ana kwao na hakuna shida yoyote, Wema atarudi nyumbani hapa na kuendelea na maisha yake kama kawaida,” alisema mama Wema.
NDOA YAO WATAFUNGIA CHUMBANI
Akizidi kutiririka, mama wa staa huyo alisema kama Diamond atamuoa Wema (kitu ambacho hakiamini kabisa) basi ndoa hiyo itafungiwa chumbani na upande wa Diamond tu ndiyo watakaoshiriki lakini upande wake hakuna atakayehudhuria.
“Ndoa yao watafungia chumbani, si hadharani tena wakiwa ndugu wa upande mmoja tu wa Diamond, sisi hatuwezi kushiriki ng’oo, ndugu zangu wakijitokeza tu nitakuwa na panga mkononi, watakiona cha moto,” alisema mama huyo.
DIAMOND, WEMA
Juzi, Diamond alipigiwa simu zake zote za mkononi lakini hakuna iliyopokelewa, akatumiwa meseji yenye madai yote, hakujibu.
Kwa upande wake, Wema alisema mama yake ametoa maoni yake kama ambavyo angeweza kutoa mzazi yeyote katika mtazamo wake.
No comments:
Post a Comment