MAREHEMU STEVEN KANUMBA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KWA HESHIMA KUBWA, KWELI ALIKUWA MTU WA WATU
Waombolezaji wa msiba wa Marehemu Steven Charles Kanumba wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu kwenye kaburi, tayari kwa kumpumuzisha katika nyumba ya milele kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo jioni , Kanumba atakumbukwa kwa kazi yake nzuri katika tasnia ya filamu hapa nchini, ambapo alijitangaza na kuitangaza nchi vyema ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kupitia filamu zake nyingi alizoigiza.
(MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN)
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa na ndugu wa karibu wakiaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho makaburini Kinondoni.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiuaga mwili wa mwanaye kwa mara ya mwisho kabla ya kuzikwa rasmi katika makaburi ya Kinondoni.
Mwanamitindo maarufu mtanzania anayefanya kazi zake za mitindo nchini Marekani Millen Magese akienda kuweka shada la Maua kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba.
No comments:
Post a Comment