Thursday, April 12, 2012

LULU KAFUTA NDOTO ZA STEVEN KANUMBA KUWA MBUNGE


Hayati Steven charles Kusekwa Kanumba gwiji la filamu alieuwawa hivi karibuni nyumbani kwake sinza maeneo ya vatican,ndoto za msanii huyu kuwa mwanasiasa mashuhuri zilitoweka baada ya mtuhumiwa Lulu kudaiwa kumua wakiwa chumbani kwake.

Steven Kanumba alikuwa na mkakati wa kugombea ubunge mkoani shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Democrasia na maendeleo (CHADEMA) na alikuwa mfuasi wa chama hiko kwa siri kubwa na hakutaka watu wajue hususani viongozi na wanachama wa (CCM) kwani alikuwa nao karibu sana na hakutaka kuaribu ukaribu nao mapema kabla hakijafika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015.
Kanumba alikuwa ni rafiki(best friend) na msiri wa Magese kwani alikuwa kanizoea kiasi cha kuniambia mambo mengi hususani maisha na maswala ya mahusiano kati yake na watu aliokuwa nao katika nyakati tofautitofauti The great alikuwa hanifichi kitu panapo ukweli aliniambia bila woga tena aliniambia nisimwambie mtu kuhusu jambo hili wala nisiandike kwenye blog kabla wakati haujafika,ila leo nimeamua kusema kwakua rafiki yangu hayupo tena duniani.

Kwa mujibu wa Marehemu Kanumba alipewa msukumo zaidi wa kuanza kujiandaa kua mgombea ubunge kwa tiketi ya (CHADEMA) na Mh.Zitto kabwe ambae ni rafiki mkubwa wa marehemu Steven kanumba,nasehemu ambayo kanumba alikuwa kanuia kujitosa kichwa-kichwa ni nyumbani kwao Shinyanga sehemu ambayo ndiko chimbuko lake.

Pamoja na kuhamasika kwa mchakato wa kuwania ubunge 2015 kanumba aliniambia hivi "kaka hata kama nikiwa mbunge siachi kutoa movie ntakua najitaidi japo nitoe hata moja tu kwa mwezi,kipindi ambacho ntakuwa siko bungeni ntapiga shooting(clip) zakufa mtu..nyingi ili nikiingia mjengeni naedit tu" alimaliza steven.

Kanumba hakutaka watu wengi wajue adhima yake hii ya kuwa mbunge 2015 kwani alijua akisema mapema watu wangemvunja moyo,wengine wangeanza kumwalibia mapema na hakutaka kuitarafiana na viongozo wa CCM mapema ambapo wengi wao ni viongozi wa juu na wengi wao hukaa nao vikao nyeti na humwamini sana kuwa ni mwanachama wa CCM.

Marehemu aliniambia maneno haya nyumbani kwake Sinza Vatcan moja ya siku ambapo aliniita nyumbani kwake tukaongea sana kama ilivyokuwa desturi yetu siku akiniona hunipa michapo mingi hasa yale mambo yetu ya ujana zaidi.

Magese ntamkumbuka sana Kanumba kwani ni kati ya watu walionisapoti sana katika harakati zangu watanzania wengi wanakumbuka hii,kashatoa fedha nyingi,muda mwingi katika harakati zangu na hakuitaji nimlipe hata shilingi moja toka kwangu,alinithamini kama ndugu yangu wa damu.
Moja ya kauli ambayo sitaisahau aliniambia "Ndugu yangu magese fanya kazi kwa bidii jitume usikate tamaa....hata kama ungekuwa mfagiaji....fagia kwa moyo na uipende kazi yako kwani katika kufagia vizuri ipo siku unaweza kuchaguliwa mfagia ikulu...katika kufagia huko utakuwa umeinuliwa toka ngazi moja kwenda nyingine" alisisitia The great.

R.I.P STEVEN KANUMBA , amen.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...