AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA KUNUNUA MBOGA, MATUNDA KWA MTANDAO
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake za Airtel Money kwa kushirikiana na kampuni ya kusambaza mboga na matunda ya Stake Agrobase International Ltd leo imezindua huduma ya kisasa iitwayo ‘Nunua mboga kwenye intanet na Airtel Money’ ambapo mteja ataweza kuagiza mboga na matunda kupitia tovuti ya www.sailfv.com na kufikishiwa alipo.
Akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya ofisi za kampuni hiyo, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando, alisema wateja wa huduma hiyo sasa wataondokana na usumbufu wa kuzunguka kwenye masoko na kuweza kuiagizia mboga na matunda kwa familia zao wakiwa nyumbani, ofisini au safarini.
No comments:
Post a Comment