Thursday, March 1, 2012

USIKU WA ‘VIDOLE JUU’ HAKUNAGA ZAIDI YA  DAR LIVE

TAMASHA la Usiku wa Vidole juu ambalo kwa sasa linafanyika kila siku ya Jumatano ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaa, usiku wa kuamkia leo lilifana vilivyo kufuatia baadhi ya wapenzi wa miondoko ya Taarab kufurika kwa ajili ya kupata burudani hiyo ukumbini hapo.

Maraha hayo yaliongozwa na New Zanzibar Stars Modern Taarab ikiwa sambamba na Kings Modern Taarab, Zanzibar Njema Modern Taarab na Super Shine Mordern Taarab.

Burudani hizo zilianza saa 3:00 usiku, ambapo kila kundi lilipata fursa ya kupiga nyimbo tano.

Kwa mujibu wa mratibu wa onesho hilo, Juma Mbizo, Jumatano ijayo Zanzibar Modern Taarab na Super Shine Modern Taarab zitatumbuiza.

Kiongozi wa Zanzibar Njema, Ahmed Mgendi, akiwa kazini.

Waimbaji wa bendi ya Zanzibar Njema wakiwajibika.



Ahmed Mgeni akiserebuka. 
 

Mwimbaji wa Kings Modern Taarab, Hassani Ally akipagawisha.



Mwimbaji wa kike wa Kings Modern Taarab akiwa na mcheza kiduku wao.

Baadhi ya mashabiki wakiserebuka.



Wacheza kiduku wa Kings Modern Taarab.

Mwimbaji wa New Zanzibar Stars Modern Taarab, Mwanamkuu, akipeleka ujumbe kwa mashabiki zake.

Waimbaji wa New Zanzibar Stars.

Mwimbaji wa Super Shine Modern Taarab, Hassani Zumu, akichapa kazi.



Baadhi ya mashabiki wakiwajibika.

Mambo ya mwambao yalivyokuwa.








No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...