Tuesday, August 16, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA DK. KIGWANGALLA ALIPOFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KITUO CHA CHESA



Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi  Kigwangalla, jana alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha COMMUNITY HEALTH EDUCATION SERVICES AND ADVOCACY- (CHESA) kilichopo Upanga, Wilayani  Ilala, jijini Dar es salaam.

Ziara hiyo ya kushtukiza inafuatia baada ya hatua ya Naibu Waziri huyo wa Afya  Dk.Kigwangalla  kuendelea kufanya ukaguzi wa Asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zikiwemo NGO’s na CBO zenye makosa ya kiutendaji na kimfumo  ambayo ni tofauti na taarifa zao katika usajili wa Serikalini na namna ya uendeshaji wa  wao.

Mbali na hayo kituo hicho cha CHESA kinashukiwa kuhusika na vitendo vya uhamasishaji wa mahusiano ya mapenzi ya Jinsia moja (USHOGA), ambayo ni kinyume na mila na Desturi za kitanzania pamoja na Katiba na sharia za Nchi.

“Mahusiano ya jinsia moja si kinyume na mila na desturi zetu tu. Bali hata sheria na katiba ya nchi yetu haziruhusu mfumo huo wa kimahusiano”  amesema  Dk..Kigwangalla

Aliendelea kubainisha kuwa: “Sisi kama Serikali hatujawahi kusaini mikataba yoyote ya kimataifa inayoruhusu  ushoga hivyo kwa taasisi yoyote hapa Nchini inayofanya hivyo ni kuvunja sheria za Nchi na inapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria na hata kufutiwa usajili wake” aliongeza Dk. Kigwangalla.

Katika ukaguzi wa kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla  akiwa ameambatana na Kaimu Msajili wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Wizara anayoiongoza, Bw. Julius Mbilinyi pamoja na Mkuu wa Upelelezi  Mkoa wa Ilala, Hassan Selengu  pia wamefanya ukaguzi katika kituo hicho ili kubaini kama kuna uwepo wa vilainishi vinavyotumiwa na watu wenye mahusiano ya jinsia moja ambavyo hivi karibuni Serikali ilipiga marufuku matumizi yake hapa nchini.
 










“Serikali ilikifuta kituo cha ‘SISI KWA SISI’ kwa sababu kilihusika na tuhuma za ushawishi wa mahusiano ya jinsia moja ambacho pia wewe ulikuwa Mkurugenzi wake. Sasa tumeamua kuchunguza na kituo hichi ili tujue kama mnahusika na vitendo hivyo ili tuchukue hatua endapo itabainika ama la” ameeleza Dk. Kigwangalla.

Aidha, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amemtaka Mkuu wa upepelezi  Bwana Hassan Selengu afanye uchunguzi wa kina katika kituo hicho ili kubaini pesa za misaada katika kituo hicho zinatokea wapi lakini pia ni kubaini kama kituo hicho kinajihusisha na ushawishi wa watu kujiunga na mahusiano ya jinsia moja.

“Tunawasiwasi kuwa mnapokea pesa nyingi  na misaada mingi kutoka katika Taasisi mbalimbali lakini pesa hizo zinatumika kuhamasisha mapenzi na mahusiano ya jinsia moja.

Mbali na hayo.  taarifa za usajili wa kituo hichi zinakinzana na malengo na miradi inayofanyika hapa.  Pia ipo miradi mbalimbali ambayo haijasajiliwa wala hujaitaja katika maelezo yako  lakini inafanyika katika kituo hichi” alihoji  Dk. Kigwangalla huku akimtajia baadhi ya miradi hiyo ambayo Serikali inaitambua.

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).

MADAI YA MANJI KUJIUZULU, MZEE AKILIMALI AMEAMUA KUWAOMBA RADHI WANAYANGA



Wakati sekeseke la Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kudaiwa kujiuzulu nafasi yake hiyo, mwanachama mkongwe wa klabu hiyo, Ibrahim Omary Akilimali maarufu kwa jina la Mzee Akilimali ametoa kauli tata juu ya sakata hilo.

Wakati huu ambapo Manji hatatoa tamko lolote juu ya uamuzi wake huo wa kujiuzulu, Mzee Akilimali amenukuliwa akisema kuwa kuna watu wa Yanga wamemuita ili kuzungumza kuumaliza mvutano unaoendelea ambapo inaelezwa kuwa mzee huyo amechangia maamuzi ya Manji kujiondoa Yanga kutokana na kumshutumu kwa maneno mengi.

Akihojiwa na kituo cha Radio ha EFM, muda mfupi uliopita Mzee Kilimali alinukuliwa akisema: “Msitake kuyakuza haya mambo, subirini kwanza nataka tuyamalize, mimi wameniita ndiyo maana nipo huku ili kuyamaliza.”

Alipoulizwa yupo wapi na ameitwa na nani, Akilimali alizema: “Nimekwambia nimeitwa huku, wewe subiri kwanza tuyamalize kisha utanipigia, subiri baada ya nusu saa nitakubeep unipigie.”

Licha ya kuendelea kubanwa kufafanua zaidi juu ya kinachoendelea, mzee huyo alisisitiza kuwa apigiwe simu baadaye na kukata simu.

Mzee Akilimali ni mzaliwa wa Kigoma, ambapo anadai alianza kuipenda Yanga tangu miaka ya 1950.

Baadaye alipopigiwa simu mzee huyo alisikika kama mtu ambaye amepoa na kuwa mpole ambapo alisema anawaomba radhi Wanayanga kama atakuwa amewakosea kwa kauli zake lakini nia yake ni kuitaka Yanga iwe moja na Manji aonyeshe heshima kwa wazee wa klabu hiyo.

“Manji ni kijana wetu, sisi wazee nikiwemo mimi tulichangia yeye kuingia ndani ya Yanga, hata mimi ndiye niliyemkabidhi ngao ya uchifu wa Yanga, sasa hapo katikati alikuwa hatushirikishi sisi wazee kama ilivyokuwa zamani.
 

“Akawa anafanya maamuzi anayoyajua yeye, nia yetu sisi wazee ni kuifanya Yanga iwe moja kuwe na mshikamano, unajua Manji ametutoa mbali, sisi ni Yanga moja, kwa mapenzi yangu yote nataka Yanga iwe kitu kimoja. Yanga ni moja na hakuna mpasuko.

CHANZO: SALEHJEMBE

HIVI NDIVYO HALI ILIVYO MAKAO MAKUU YA YANGA BAADA YA MANJI KUJIUZULU

Kutokana na taarifa kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuamua kujiuzulu katika nafasi hiyo, kumekuwa na hali ya sintofahamu ndani ya klabu hiyo, hizi ndivyo pichani hali halisi ilivyo ndani ya makao makuu ya klabu hiyo muda mupi uliopita.

Ambapo wanachama na wapenzi wa timu hiyo wamekusanyika wakijadiliana juu ya majaaliwa ya klabu yao.



Monday, August 15, 2016

BAADA YA TAARIFA YA MANJI KUJIUZULU, WANAYANGA WATIKISIKA



Mapema leo kuliibuka taarifa kuwa Yanga inaweza kumpoteza mwenyekiti wake Yusuf Manji ambaye inadaiwa kuwa anataka kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake.
  




Habari hiyo imekuwa ikisambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali na mmoja wa viongozi wa Yanga alikiri kuwa suala hilo lipo.

Licha ya taarifa hizo kusambaa kwa kasi bado hakuna taarifa rasmi kuwa kiongozi huyo amechukua uamuzi huo zaidi ya tetesi.

Kwa mujibu wa mtandao wa salehjembe.blogspot.com, Manji amenuukuliwa akisema kuwa anataka aachwe na hataki kujibu hoja hiyo kama kweli amejiuzulu au la.

Baada ya taarifa hiyo kuendea Wanayanga wengi wamekuwa na maoni tofauti wapo wanaolalamika kuwa Manji ni mkombozi wao hasa katika masuala ya fedha na wengine wanadai anaweza kuondoka tu kwa kuwa msaada wake umefikia ukomo. Mjadala unaendelea.

USAIN BOLT ALIVYOWEKA REKODI OLIMPIKI RIO 2016



Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ameandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda medali  ya dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika mbio za mita 100, kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio 2016.

Bolt, 29, amechukua muda wa sekunde 9.81 katika fainali yake ya mwisho katika michezo ya olimpiki, kwa kuiga ushindi sawa na huo katika michezo ya olimpiki mjini Beijing 2008, na London 2012.

Gatlin, ambaye amepigwa marufuku mara mbili kwa matumizi ya dawa za kutitimua misuli, alimaliza sekunde 0.08 nyumna ya Bolt na kuchukua nishani ya fedha.

“Nilitarajia kwenda kasi zaidi, lakini nafurahia kwamba nimeshinda,” Bolt ameiambia BBC.
Mwanariadha wa Canada Andre de Grasse ameshinda nishani ya shaba, na kuandikisha muda bora wa kibinafsi wa sekunde 9.91, mbele ya mwanariadha wa Jamaica Yohan Blake.

Bolt anatazamia kuondoka Rio na nishani zaidi za dhahabu katika mbio za mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti, jinsi ilivyokuwa katika michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.

Mwanariadha huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 alisema kuwa atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa dunia mwaka 2017.






POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...