Wakati
sekeseke la Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kudaiwa kujiuzulu nafasi yake
hiyo, mwanachama mkongwe wa klabu hiyo, Ibrahim Omary Akilimali maarufu kwa
jina la Mzee Akilimali ametoa kauli tata juu ya sakata hilo.
Wakati huu
ambapo Manji hatatoa tamko lolote juu ya uamuzi wake huo wa kujiuzulu, Mzee
Akilimali amenukuliwa akisema kuwa kuna watu wa Yanga wamemuita ili kuzungumza
kuumaliza mvutano unaoendelea ambapo inaelezwa kuwa mzee huyo amechangia maamuzi
ya Manji kujiondoa Yanga kutokana na kumshutumu kwa maneno mengi.
Akihojiwa na
kituo cha Radio ha EFM, muda mfupi uliopita Mzee Kilimali alinukuliwa akisema:
“Msitake kuyakuza haya mambo, subirini kwanza nataka tuyamalize, mimi wameniita
ndiyo maana nipo huku ili kuyamaliza.”
Alipoulizwa
yupo wapi na ameitwa na nani, Akilimali alizema: “Nimekwambia nimeitwa huku,
wewe subiri kwanza tuyamalize kisha utanipigia, subiri baada ya nusu saa
nitakubeep unipigie.”
Licha ya
kuendelea kubanwa kufafanua zaidi juu ya kinachoendelea, mzee huyo alisisitiza
kuwa apigiwe simu baadaye na kukata simu.
Mzee
Akilimali ni mzaliwa wa Kigoma, ambapo anadai alianza kuipenda Yanga tangu
miaka ya 1950.
Baadaye
alipopigiwa simu mzee huyo alisikika kama mtu ambaye amepoa na kuwa mpole
ambapo alisema anawaomba radhi Wanayanga kama atakuwa amewakosea kwa kauli zake
lakini nia yake ni kuitaka Yanga iwe moja na Manji aonyeshe heshima kwa wazee
wa klabu hiyo.
“Manji ni
kijana wetu, sisi wazee nikiwemo mimi tulichangia yeye kuingia ndani ya Yanga,
hata mimi ndiye niliyemkabidhi ngao ya uchifu wa Yanga, sasa hapo katikati
alikuwa hatushirikishi sisi wazee kama ilivyokuwa zamani.
“Akawa
anafanya maamuzi anayoyajua yeye, nia yetu sisi wazee ni kuifanya Yanga iwe
moja kuwe na mshikamano, unajua Manji ametutoa mbali, sisi ni Yanga moja, kwa
mapenzi yangu yote nataka Yanga iwe kitu kimoja. Yanga ni moja na hakuna
mpasuko.
CHANZO:
SALEHJEMBE
No comments:
Post a Comment