Saturday, May 17, 2014

DIAMOND AFUNIKA KWENYE MBIO ZA KUELEKEA KWENYE TUZO ZA MTV BILICANAS


Diamond akizungumza jambo mbele ya watu waliokusanyika ndani ya Ukumbi wa Billicanas
Staa wa wimbo wa Number One, Nasibu Abdul 'Diamond', jana alikuwa ndani ya Ukumbi wa Billicanas kuzungumzia juu ya hatua kubwa aliyopiga hadi kuwepo katika Tuzo za MTV ambazo zinatarajiwa kufanyika hapo baadae mwaka huu.

Diamond na wasanii wengine kama Sauti Soul kutoka Kenya walikuwepo ndani ya ukumbi huo ambapo mbali na kuzungumzia furaha ya kuteuliwa, baadaye wasanii mbalimbali ambao wameteuliwa katika kinyanganyiro hicho walitumbuiza mmoja baada ya mwingine.
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali waliokusanyika ndani ya ukumbi huo.
Muigizaji Wema Sepetu akihojiwa na mwandishi wa habari ndani ya ukumbi huo kuhusiana na uteuzi wa Diamond kuwania Tuzo za MTV.Kulia ni mwigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel.
Wasanii kutoka Kenya, Sauti Soul wakitumbuiza ndani ya Ukumbi wa Billicanas
Diamond akiwaburudisha mashabiki waliofurika ukumbini humo.
Mashabiki wakiburudika vilivyo ndani ya Ukumbi wa Bilicanas ambapo Diamond na wasanii wengine walikuwa wakifanya yao.

Tuesday, May 13, 2014

WANAMUZIKI 5 TWANGA HOI KWA DENGUE

Stori: Musa Mateja
HOMA ya Dengue imezidi kuwa tishio jijini Dar es Salaam, ambapo wanamuziki watano wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, wamekumbwa na ugonjwa huo, habari zimefika katika dawati la Risasi Mchanganyiko.


Mmoja wa wanamuziki wa Twanga anayesumbuliwa na Homa ya Dengue, Bakari Kasongo ‘Mandela’.

Mtoa habari Hassan Rehani ambaye ni meneja wa bendi hiyo, alizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni na kuwataja wanamuziki hao kuwa ni Badi Bakule, Ramadhan ‘Pentagoni’, Bakari Kasongo ‘Mandela’, Sabrina Mbetembete na Natalia Mbui.

“Nimeshitushwa sana na ugonjwa huu, maana katika maisha yangu ugonjwa ambao nilishawahi kuona unasumbua watu wa sehemu moja kwa wingi kiasi hiki ni Kipindupindu tu, sasa hii dengue ni hatari,” alisema Rehani na kuongeza kuwa wanamuziki hao walikuwa wamelazwa Hospitali ya Mwananyamala na kwamba hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.

Naye mmoja wa wagonjwa hao, Rama Pentagoni, alipozungumza na mwandishi wetu alisema anaendelea vizuri, huku akiuelezea ugonjwa huo kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu.

ROSE NDAUKA AZIDI KULILIA NDOA

STAA wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amezidi kulilia ndoa ambapo sasa ameonesha shauku ya kufunga hata ndoa ya mkeka ili kukata kiu yake ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu.


Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka.

Rose aliyejifungua hivi karibuni huku baba wa mtoto akijulikana kwa jina moja la Malick alisema hayo hivi karibuni nyumbani kwake Magomeni, Dar, ambako alikutana na mwandishi wetu aliyetaka kujua ndoa ya msanii huyo itafungwa lini?

“Nimeshasubiri sana, nimejiandaa kwa kila kitu hata upande wa dini niko tayari kwenda sambamba na mume wangu mtarajiwa, naamini siku chache zijazo nitaolewa,” alisema Rose ambaye uchumba wake umekuwa ukifunikwa na sintofahamu kibao.

Rose aliongeza kuwa siku atakayofunga ndoa furaha yake itakuwa mara dufu kwa sababu tayari ana ‘baby’.

HATARI: JENGO LAPOROMOKA HUKO ZANZIBAR, TAZAMA PICHA ZOTE HAPA





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijumuika pamoja na baadhi ya wananchi kuangalia athari iliyojichomoza kwenye nyumba ya Bwana Salim Ahmed Salim baada ya ukuta na dari yake kuanguka saa sita usiku juzi mkabala na Skuli ya Sekondari ya Tumekuja Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

Athari ya nyumba iliyobomoka hapo Mtaa wa Vuga ilisababisha usumbufu wa watumiaji wa Bara bara itokayo Vuga kuelekea Shangani au Serena na kulazimika kufungwa kwa bara bara hiyo..(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).
---------
Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar, Jeshi la Polisi pamoja na Mamlaka ya Usafiri zimekumbushwa kuendelea kuzuia uingiaji wa gari kubwa zenye uzito wa zaidi ya Tani Mbili katika eneo la Mji Mkongwe ili kunusuru majengo yaliyono ndani ya mamlaka hiyo.

Kumbusho hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofanya ziara fupi kukagua athari ya nyumba iliyoporomoka ukuta na Dari yake juzi usiku iliyopo Mkabala na Skuli ya Sekondari ya Tumekuja Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

Balozi Seif alisema ukaidi wa baadhi ya madereva wa gari kubwa kupitisha Gari gari zao katika eneo hilo umesababisha uchafuzi wa mandhari na haiba ya Mji mkongwe wa Zanzibar ambao hivi sasa uko katika urithi wa Kimataifa.

“ Jeshi la Polisi wakati huu litahitajika kuwa na kazi ya ziada katika kuhakikisha agizo lililotolewa na Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar linatekelezwa ipasavyo “. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimpa pole Mmiliki wa Nyumba hiyo Bwana Salim Ahmed Salim kwa hasara aliyoipata alimtaka kuwasiliana na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar katika juhudi zaujenzi wa nyumba hiyo utakaozingatia mpango halisi wa uhifadhi wa Mji huo.

Akitoa ufafanuzi wa athari nyingi zilizojitokeza ndani ya nyumba za Mji Mkongwe, Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utafiti cha Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Bibi Madina Haji Khamis alisema ujenzi usiozingatia utaalamu wa Mamlaka husika pamoja na upitishwaji wa gari kubwa ndio sababu kubwa za msingi za athari hizo.

Bibi Madina alifahamisha kwamba baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo walikuwa wakipandishia kuta wakati wa ujenzi au matengenezo zaidi ya uwezo wa msingi wa nyumba hizo hali inayoleta athari ya mipasuko ya nyumba hizo sambamba na mitetemeko ya gari kubwa zinazopitishwa pembezoni mwa nyumba hizo.

Mapema Mmiliki wa Nyumba hiyo Bwana Salim Ahmed Salim alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba dalili za kuanguka kwa jengo hilo zilijionyesha mapema kutokana na kuvimba na baadaye kupasukwa kwa eneo la mbele la ukuta wa nyumba hiyo.
Bwana Salim alifahamisha kwamba kutokana na hali hiyo alilazimika kuuarifu Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar uliolazimia baadaye kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kuchukuwa hatua za kuifunga bara bara hiyo.

“ Nilijaribu kuufuata Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe uniruhusu kuifanyia matengenezo makubwa nyumba yangu ili baadaye niitumie kwa makazi na familia nyangu lakini bado sijapata jibu na huku inaporomoka “. Alieleza Bwana Salim Ahmed Salim.
Nyumba hiyo ya ghorofa moja mpaka inaporomoka ukuta na dari yake majira ya saa sita juzi usiku lakini hamna watu waliokuwa wakiishi ndani yake.

Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi nyengine zimelazimika kuzuia Gari zote zinazotumia Bara bara hiyo kutoka Vuga kuingia Shangani au kupitia Serena ili kujaribu kuepuka hatari katika kipindi hichi cha Mvua za Masika.

Kwa mujibu wa hali halisi ilivyo hivi sasa gari zote zinazokusudia kuingia ndani ya eneo la Mamlaka ya Mji Mkongwe zinalazimika kutumia Bara bara itokayo Malindi na zisizidi uzito wa zaidi ya Tani mbili.

Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kwa miaka kadhaa sasa imo ndani ya Ramani ya Dunia ya urithi wa hifadhi ya Kimataifa chini ya usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni { UNESCO }.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana kwa mazungumzo na ujumbe wa Kampuni ya uwekezaji vitega uchumi vya sekta za Afya, Kilimo, Umeme, viwanda vidogo vya mazao ya Baharini ya Lucky Exports kutoka Nchini India.

Kampuni hiyo ambayo imefungua Matawi yake katika mataifa mbali mbali Barani Afrika tayari imeshapata usajili wa kufungua Tawi lake Nchini Tanzania.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar Meneja wa Kampuni hiyo Bwana Ravi Rai alisema Taasisi yake imelenga kutoa huduma za afya pamoja na viwanda vidogo vidogo vya mazao ya Baharini.

Bwana Ravi Rai alisema wakati Uongozi wa Taasisi yake ukisubiri kuanza na hatimae kukamilisha taratibu zote za uwekezaji uwekaji wa miradi hiyo umekusudia kusaidia kutoa ajira kubwa kwa wazalendo pamoja na kuongeza mapato ya Taifa.

Alifahamisha kwamba utafiti wa wataalamu wa Taasisi hiyo utafanywa ili kuangalia miradi ambayo kampuni hiyo inaweza kuiwekeza hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

“ Tunafarajika kuona kwamba miradi yoyote tutakayoamuwa kuitekeleza kwenye uwekezaji wa mataifa mbali mbali duniani na hasa tukilenga zaidi Bara la Afrika inafadhiliwa na Serikali ya India “. Alisema Meneja huyo wa Lucky Exports.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema miradi iliyofikiriwa kuanzishwa na Uongozi wa Kampuni hiyo hapa Zanzibar ya Sekta ya Afya na Viwanda Vidogo vidogo vya mazao ya Baharini itasaidia kustawisha maisha naustawi wa Jamii Nchini.

Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Kampuni hiyo ya Lucky Exports kutoka Nchini India kurahisisha maombi yao ya uwekezaji ili taasisi zinazohusika na uwekezaji ziweze kuyapitia na kutoa maamuzi yanayostahiki kwa wakati muwafaka.

Kampuni ya Uwekezaji ya Lucky Exports ya Nchini India ambayo tayari imeshafungua matawi yake katika Mataifa ya Ethiopia, Guinea Bisau, Malawi na Tanzania inajihusisha zaidi na uwekezaji wa miradi ya Afya, Kilimo, Viwanda vya mazao ya Baharini, Umeme pamoja na huduma za Reli.

NABII DR. LUCY NATASHA KUFUNDISHA AKINA MAMA NA MABINTI KATIKA KANISA LA RGC TABATA CHANG'OMBE KWA MTUME PETER NYAGA


Watanzania umefika wakati wa kubanan kwa Yesu Kristo katika kanisa la RGC Tabata Chang'ome kwa Mtume anayetikisa hapa mjini Mtume Peter Nyaga. Mungu ameamua kuongea na akina mama na mabinti katika kongamano litakaloongozwa na watumishi wa Mungu wapatao nane wakivamia madhabahu moja huku wakitumia MIC moja siku hiyo.

Kilichonifurahisha ni pale Nabii mrembo aliyeumbika vizuri kwa kazi ya Mungu kutoka Kenya Nabii Dr. Lucy Natasha ambaye amehubiri sehemu nyingi sana duniani. Nabii huyu amepewa kazi na Mungu ya kuwaleta kuwakomboa waliopotea na kuhakikisha waliokombolewa wanaziidi kufurahi ukombozi wao mpaka siku ile ya mwisho. Jukumu lake ni kuhakikisha anafanya kila awezalo kumtukuza Mungu wetu na kutagaza habari njema za Mungu.

Nabii Dr. Lucy Natasha (Kenya)

Usikose kabisa mwana wa Mungu katika kongamano hili lenye waimbaji zaidi ya kumi kuvamii madhabahu moja kwaajili yako wewe UBARIKIWE. Mtaarifu na jamaa yako ili siku hiyo ashuhudie ishara na miujiza ya BWANA..
Mtume Peter Nyaga na mke wa Mchungaji Anna Nyaga wamejipanga kabisa kuhakikisha huu ugeni utakaofika katika kanisa lake utakuwa salama. Na eneo la kanisa lake kuzungukwa na nguvu za Mungu zitakazokuhamisha wewe katika mazingira uliyozoea na kuingia katika mazingira mengine tofauti.

Waimbaji kama Sarah Mvungi, Madam Ruti, Masanja Mkandamizaji, Mess Jacob Chengula, Martha Mwaipaja, Neema Gasper na wengine wengi watahakikisha kazi ya BWANA wetu YESU KRISTO inajidhihirisha kwako wewe utakayefika siku hiyo.

Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851523

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...