Watanzania
umefika wakati wa kubanan kwa Yesu Kristo katika kanisa la RGC Tabata
Chang'ome kwa Mtume anayetikisa hapa mjini Mtume Peter Nyaga. Mungu
ameamua kuongea na akina mama na mabinti katika kongamano
litakaloongozwa na watumishi wa Mungu wapatao nane wakivamia madhabahu
moja huku wakitumia MIC moja siku hiyo.
Kilichonifurahisha
ni pale Nabii mrembo aliyeumbika vizuri kwa kazi ya Mungu kutoka Kenya
Nabii Dr. Lucy Natasha ambaye amehubiri sehemu nyingi sana duniani.
Nabii huyu amepewa kazi na Mungu ya kuwaleta kuwakomboa waliopotea na
kuhakikisha waliokombolewa wanaziidi kufurahi ukombozi wao mpaka siku
ile ya mwisho. Jukumu lake ni kuhakikisha anafanya kila awezalo
kumtukuza Mungu wetu na kutagaza habari njema za Mungu.
Nabii Dr. Lucy Natasha (Kenya)
Usikose
kabisa mwana wa Mungu katika kongamano hili lenye waimbaji zaidi ya
kumi kuvamii madhabahu moja kwaajili yako wewe UBARIKIWE. Mtaarifu na
jamaa yako ili siku hiyo ashuhudie ishara na miujiza ya BWANA..
Mtume
Peter Nyaga na mke wa Mchungaji Anna Nyaga wamejipanga kabisa
kuhakikisha huu ugeni utakaofika katika kanisa lake utakuwa salama. Na
eneo la kanisa lake kuzungukwa na nguvu za Mungu zitakazokuhamisha wewe
katika mazingira uliyozoea na kuingia katika mazingira mengine tofauti.
Waimbaji
kama Sarah Mvungi, Madam Ruti, Masanja Mkandamizaji, Mess Jacob
Chengula, Martha Mwaipaja, Neema Gasper na wengine wengi watahakikisha
kazi ya BWANA wetu YESU KRISTO inajidhihirisha kwako wewe utakayefika
siku hiyo.
Tangazo limetengezwa na Rumafrica +255 715 851523
No comments:
Post a Comment