Thursday, February 28, 2013

JOHN MNYIKA.....NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAWO WA UMEME, SERIKALI IELEZE WANANCHI UKWELI NA HATUA KUHUSU UDHAIFU KWENYE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA DHARURA



Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012.


Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.


Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo.


Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.




Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme.


Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012.


Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika.


Wenu katika uwakilishi wa wananchi,


John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

MSANII OMOTOLA ANG'AA HOLLYWOOD


 
Muigizaji wa Nollywood, Omotola, Jalade- Ekeinde, ameanza kuonekan kwenye televisheni za Marekani, kwenye kipindi kiitwacho Bounce

Nyota huyo ambaye amekuwa Marekani kwa muda sasa ameanza kuonyesha uwezo wake mbele ya wakali wa Hollwood nchini Marekani

Baadhi ya wasanii mbalimbali kutoka Nigeria walishindwa kung'aa lakini msanii huyo amefanikiwa kushiriki kwenye tamthilia nchini Marekani

Katika tamthilia hiyo Omotola amecheza na Kimberly Elise

NIKKI MBISHI ASALUTI KWA LADY JAYDEE




Nikki Mbishi ni rapper usiyeweza kumfananisha na yeyote Tanzania kwa uwezo wake usioelezeka katika uandishi wa haraka wa mashairi yenye mistari konde na uwezo wa kufanya mitindo huru (freestyle). Pia ana kumbumbuku ya ajabu na akiwa na uwezo wa kuimba nyimbo za wakongwe kama Profesa Jay na hata wa Marekani utadhani kaziandika yeye.
Lakini pamoja na maisha yake ya muziki kuzungukwa zaidi na utamaduni wa Hip Hop, Nikki aka Terabyte huchukua muda pia kusikiliza muziki laini wa wasanii wenzake wa Bongo na kwa mtazamo wake Lady Jaydee ndiye msanii wa kike anayemkubali kuliko yeyote.

“Leo nimeamka na dada mkuu tu @JideJaydee hakuna kama huyu kwenye historia ya wanamuziki wa kike Bongo @GraceMatata fuata huyo dada.,” ametweet Nikki Mbishi.

Rapper huyo controversial ameendelea kutweet majina ya nyimbo kibao za nguli huyo wa muziki wa Tanzania ambaye jina lake halisi ni Judith Mbibo.

"MIMI SI MGONJWA.."...RAY AFUNGUKA


Picha hiyo ya kushoto inamuonesha alivyokuwa mwanzo..na kulia na jinsi alivyo sasa
------------




Muigizaji aliyepo kwenye list A ya waigizaji wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi aka Ray ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia anaumwa kutokana na kupungua mwili wake kwa kiasi kikubwa.

Ray amezikanusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo gazeti la udaku la Kiu wiki hii lilikuwa na habari isemayo, ‘Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa.

Hata hivyo Ray amesema hali hiyo imetokana na kufanya mazoezi zaidi siku za hivi karibuni. “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.

ALAMA JABIR AKERWA NA MGAO WA UMEME


S










Siku za hivi karibuni kumekuwepo na katizo la umeme la mara kwa mara katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kiasi cha kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi.
Kufuatia tabia hiyo ya Tanesco kufanya yao kila siku na kuwaweka wajasiriamali wanaotegemea umeme kwenye mawe, mtangazaji wa kipindi ca Mkasi, Salama Jabir, ameamua kuzipunguza hasira zake kwenye Twitter kwa kuandika:

Kazi inabidi ziende jamani…The f**k is wrong na hii nchi?!Umeme tu?????!Shida isotatulika miaka nenda rudi?!Tunachoshaaaana. F**k that shit!! Taarifa hakuna…kuunguziana mali tu,kulipa hamlipi,kauli nzuri hamna!! Who does that?! Well..Mnatufunza sana,Asanteni!!

Watu wakiamua kuishi nje serikali inalalamika Ooh vijana hawana upendo na nchi yao!!Utapendaje nchi inayokurudisha nyuma? What the f**k?! Well KZMZ!!!


Alosema bora mthamini mbwa naona hakuwa mbali na Ukweli..Ki ukweli misemo ya wahenga yote ni ukweli mtupu, again…KZMZ.

Nimejipigapiga mwenyewe nikanunua kaTV ka kitundika ukutani kama tunazoziona kwenye TV mkaunguza,nikarudisha dukani watengeneze.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...