Thursday, February 28, 2013

NIKKI MBISHI ASALUTI KWA LADY JAYDEE




Nikki Mbishi ni rapper usiyeweza kumfananisha na yeyote Tanzania kwa uwezo wake usioelezeka katika uandishi wa haraka wa mashairi yenye mistari konde na uwezo wa kufanya mitindo huru (freestyle). Pia ana kumbumbuku ya ajabu na akiwa na uwezo wa kuimba nyimbo za wakongwe kama Profesa Jay na hata wa Marekani utadhani kaziandika yeye.
Lakini pamoja na maisha yake ya muziki kuzungukwa zaidi na utamaduni wa Hip Hop, Nikki aka Terabyte huchukua muda pia kusikiliza muziki laini wa wasanii wenzake wa Bongo na kwa mtazamo wake Lady Jaydee ndiye msanii wa kike anayemkubali kuliko yeyote.

“Leo nimeamka na dada mkuu tu @JideJaydee hakuna kama huyu kwenye historia ya wanamuziki wa kike Bongo @GraceMatata fuata huyo dada.,” ametweet Nikki Mbishi.

Rapper huyo controversial ameendelea kutweet majina ya nyimbo kibao za nguli huyo wa muziki wa Tanzania ambaye jina lake halisi ni Judith Mbibo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...