Thursday, February 28, 2013

MAPACHA WATATU KUZINDUA YARABI NAFSI MARCH 2

Waimbaji wa bendi ya Mapacha watatu Khalidi Chokolaa (kushoto) na Jose Mara wakiwa wameshika CD ya albam yao mpya Dar es salaam jana watakayoizindua March 2 katika ukumbi wa bussines park.

Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wao

Msanii wa bendi ya mapacha watatu Catherine Fidelic ' Cindy' akiimba mbele ya wana habari

BABA MTAKATIFU BENEDIKTI XVI AKUTANA KWA MARA YA MWISHO NA WAUMINI ST. PETER'S SQUARE



Umati Mkubwa wa Waumini

Moja la jukwaa kubwa la wapiga picha wa kimataifa

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome alikuwepo kuiwakilisha Tanzania.

Wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma walikuwepo pia.

Baba Mtakatifu akiingia kwenye St. Peter's Square

Picha ya Baba Mtakatifu alipotupitia Karibu huku akitubariki

Bendera ya Tanzania


Baba Mtakatifu Benedikti XVI tarehe 27 Februari amekutana na waumini kwa mara ya mwisho kabla ya kung'atuka kwenye nafasi yake ya kuliongoza kanisa katoliki hapo kesho kwenye mida ya saa mbili za usiku.


Umati mkubwa wa watu ulijumuika nje ya kanisa la Mtakatifu Petro kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kuliongoza kanisa katoliki kwa kipindi cha miaka 8 tokea kuchaguliwa kwake.Itakumbukwa kuwa Baba Mtakatifu Benedikti XVI alichaguliwa kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha Baba Mtakatifu John Paul II. Mwenyezi mungu amuongoze Baba mtakatifu kwenye maisha yake yote nje ya uongozi wa Kanisa katoliki.


Jumuiya ya Watanzania Roma ikiongozwa na Katibu wake ilikuwepo kuiwakilisha Tanzania kwenye siku hii ya Kihistoria duniani. kwa picha zaidi mnaweza kutembelea hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.


Picha zote zimeletwa kwenu na Andrew Chole Mhella (Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma)

Wednesday, February 27, 2013

RIHANNA NA CHRIS BROWN WARIDHIA KUFUNGA NDOA JULY MWAKA HUU



Jarida maarufu (Star Magazine) limeripoti kwamba mastaa wa muziki Chris Brown na Rihanna wanampango wa kufunga ndoa mwishoni mwa July 2013 nyumbani kwa kina Rihanna huko Barbados.

Jarida hili limeendelea kutiririka kwamba kwenye ndoa hiyo wamepanga kusherehekea na watu mbalimbali wakiwemo wanaoamini kwamba Chris Brown amebadilika kitabia.

Ni harusi ambayo watu wote walioalikwa watakua wamesimama na wahudumu watakuepo kumfata kila mtu alipo, pia wale wachoraji wa tattoo watakuepo pia.

OMOTOLA NA GENEVIEVE NNAJ HAKUNA BEFU TENA




Stori za kuaminika kutoka kwenye ardhi ya Nigeria ni kwamba beef iliyokuepo kati ya waigizaji mastaa wa Nigeria Omotola Jalade na Genevieve Nnaji imekwisha ambapo kuonyesha kwamba uhasama umefutika Genevieve alihudhuria suprise ya pili ya birthday ya Omotola Jalade kama inavyoonekana kwenye hizi picha.

Wengine waliohudhuria ni Bimbo Akintola, Monlisa Chinda, Guild of Nigeria president Ibinabo Fiberisima, Chidi Mokeme, pamoja na mwimbaji staa wa Nigeria Banky W, Sound Sultan na wengine.



Omotola na Genevieve Nnaji.


.





.

RIPOTI KAMILI KUHUSU KUFUNGWA KWA VITUO VIWILI VYA REDIO PAMOJA NA FAINI WALIYOTOZWA CLOUDS FM



Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari  jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo

KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake  kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.

Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.


Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa

uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.


Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa kufanya.

Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa wakiviamini vituo hivyo.

Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.

Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo



POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...