Friday, March 4, 2016

MAGUFULI ATIKISA KENYA,UGANDA, RWANDA NA BURUNDI!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Arusha hawapo pichani kabla ya ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.

RAIS John Pombe Magufuli ametikisa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community) za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini kufuatia hotuba yake iliyowasisimua wananchi wengi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais Magufuli ambaye amejipatia sifa kubwa nchini kutokana na kuhimiza nidhamu kwa wafanyakazi wa serikali na uwajibikaji kwa viongozi wa umma, Jumatano hii aliwaambia viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa ni lazima wajinyime kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wao ambao ni masikini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Uganda, Yoweri Meseveni na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukipigwa kabla ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
“Huyu ndiye mtu anayestahili kuongoza mataifa kama yetu, wananchi tumefanywa masikini kwa sababu viongozi wetu wanaendekeza anasa, sijui kwa nini Mungu hakumleta mtu huyu kuwa rais wetu,” aliandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook, mtu aliyejitambulisha kama Kabaka Njiru, raia wa Uganda.
Katika mtandao wa Instagram, mtu anayejiita born2shine.thika kutoka Kenya, alisema staili ya uongozi wa Magufuli wa Tanzania inapaswa kuigwa na viongozi wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama lengo lao ni kutokomeza umasikini katika nchi zao.
“This is a leader with passion, hebu nyie wengine @Kenyatta, @Museveni, @Nkurunzinza, ingieni kwenye hii listi ya Magufuli and Kagame, we need to see new and developing East Africa, Viva Magufuli,” aliandika.
Rais Magufuli alichaguliwa kuendelea na wadhifa wa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, baada ya kumalizia kipindi cha Jakaya Kikwete aliyeondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Katika mkutano huo, alisisitiza kiongozi yeyote atakayeshindwa kutimiza majukumu yake, atamshtaki kwa rais wa nchi yake ili ‘amtumbue’.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...