Staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, na rapa maarufu wa Marekani, Kanye West.
Stori: Musa Mateja, Wikienda
DAR ES SALAAM: Kutoka Tandale hadi Marekani! Staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, melidokezea Ijumaa Wikienda kilichojiri kwa takriban dakika 20 alipokutana uso kwa uso na rapa kubwa duniani wa Marekani, Kanye West.
UWANJA WA NDEGE LOS ANGELES
Diamond alikutana na Kanye West kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles wa LAX nchini Marekani wakati akisubiri ndege kuelekea Las Vegas kwa ajili ya shoo na kazi zake za kimuziki.
Katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda akiwa Las Vegas, Diamond alisimulia alivyokutana na Kanye West na kufanikiwa kuzungumza naye tofauti na watu wengi wanavyoamini kuwa jamaa huyo siyo mtu wa ‘kuingilika’ kirahisi.
Diamond Platnumz akiwa kwenye ndege.
MAHOJIANO
Wikienda: Ilikuwaje ukaweza kupiga picha na Kanye West?
Diamond: Dah! Aisee ni kama zali vile maana sikuamini kama ni mimi mtoto wa Kimanyema nipo na Kanye West. Kwanza nilipomuona nilishtuka sana lakini nikasema piga ua, liwalo na liwe ngoja nimvae pamoja na kwamba alikuwa na timu ya kufa mtu.
Wikienda: Hukuzuiwa kumfuata na kumvaa kwa sababu tunavyojua huwa ana mabaunsa na mtu haruhusiwi kumsogelea hadi akubali mwenyewe?
Diamond: Kiukweli ilikuwa kazi sana lakini niliwafuata watu wake wakiwemo mameneja wake, nikajitambulisha ndipo wakamwambia akaitikia nimsalimie na kuongea naye.
Baada ya kuwasili Las Vegas
MAZUNGUMZO DAKIKA 20
Wikienda: Mazungumzo yenu yalichukua muda gani na mlizungumza kuhusu nini?
Diamond: Tulitumia kama dakika 20 na zaidi kwa sababu naye alikuwa anasubiri ndege lakini hasa ilikuwa ni kujitambulisha, kuwaonesha kazi zangu kwenye YouTube na kuweka mipango ambayo ni mapema mno kuiweka wazi.
Wakati nauanza mwaka huu nilisema kuwa kwa Afrika muziki wetu wa Bongo Fleva umeeleweka na mwaka huu ni zamu ya
Marekani na kweli naona milango inaanza kufunguka.
Wikienda: Unaweza kudokeza angalau kidogo mlichokubaliana?
WABADILISHANA MAWASILIANO
Diamond: Kwanza ilikuwa ni kufahamiana kisha nilibadilishana naye mawasiliano hivyo naamini mambo mazuri yanakuja.
Zaidi sana ni kuhusu muziki wetu na namna ya kujipanua kibiashara.
Wikienda: Ilikuwaje akakubali upige naye picha?
Diamond: Wakati anaondoka kwa sababu alionekana kuwa na haraka, niliwaomba mameneja wake, wakaniruhusu, si unajua tena?
Nikachomoa simu yangu fasta na kugonga naye picha. Cha msingi tuombeane Mungu mambo yaende sawia.
Wikienda: Mbali na kufanikiwa kukutana na Kanye West, una program gani nyingine huko?
Diamond: Kwanza nina shoo hapa Las Vegas kisha nitafanya video ya ngoma yangu mpya na Ne-Yo (mwanamuziki wa Marekani) ambayo tayari tulishafanya audio.
WABONGO WENGINE NA KANYE WEST
Mbali na Diamond, mastaa wengine wa Kibongo waliowahi kukutana na Kanye West na kupiga naye picha ni sexy lady wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na mwanamitindo Miriam Odema.
No comments:
Post a Comment