Thursday, March 17, 2016

Kadja Nito adaiwa kuchumbiwa


KADJA NITO (5)
Staa wa Bongo fleva Khadija Maige ‘Kadja Nito’.
Mayasa Mariwata
MWANADADA anayefanya poa kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Khadija Maige ‘Kadja Nito’ anadaiwa kuchumbiwa na kigogo mmoja (jina kapuni) hali inayomfanya kukaa kimya kimuziki.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilicho karibu na msanii huyo, bi’shosti huyo aliyekuwa akibamba na Wimbo wa Sina Maringo amekuwa akionekana viwanja mbalimbali akijiachia na kigogo huyo. “Sasa hivi mambo yake yamemnyokea, ndiyo maana siku chache zilizopita alionekana akila bata Sauzi, japo haonekani akipiga dili zozote zinazohusiana na kazi zake za kimuziki,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunasa madai hayo, Showbiz Xtra ilimvutia waya Kadja kujua kama kuna ukweli ambapo alifunguka;“Hilo la kuchumbiwa siyo kweli jamani, ni kweli sionekani kupata dili za shoo hivi karibuni lakini siyo kwamba nimefichwa na mtu, hapana! Niwaambie tu mashabiki wangu, soon mtaona mambo makubwa kutoka kwangu sababu Sauz nilienda kikazi siyo kuuza sura kama wengi wanavyodhani.”

Pokea habari na matukio ya mastaa katika simu yako

Global Publisher_17cm x 25cm_Ad1 copy

Wednesday, March 16, 2016

Wasanii Bongo Movie wampongeza Makonda


Makonda (16)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel.
Makonda (15)
Mboni Masimba akimpatia Paul Makonda zawadi ya keki.
Makonda (14)
Steve Nyerere akitoa neno katika hafla hiyo.
Makonda (13)
RC Paul Makonda akiongea na mastaa mbalimbali wa Bongo katika hafla hiyo ya kumpongeza.
Makonda (11)
Mwanamuziki Mrisho Mpoto naye akitoa nasaha zake kwa Mhe. Paul Makonda.

Tuesday, March 15, 2016

Usikose Usiku wa kuimba Maisha Basement leo....Kiingilio 5,000 tu


BETHDEI YA MWANA-FA NA BARAKA DA PRINCE MAISHA ILIVYOFANA MAISHA BASEMENT CLUB WEMA NDANI


JUMAPILI ya jana mastaa kibao wa muziki wa Bongo Fleva walihudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa msanii Baraka Da Prince na Mwana-FA iliyofanyika katika Ukumbi wa Maisha Basement ulipo Kijitonyama jijini Dar.
Sherehe hiyo ilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii Mirror, Mo Music, Ali Kiba, T.I.D, Ommy Dimpoz, Barnaba Boy na wengine kibao sambamba na burudani ya nguvu kutoka kwa DJ Ommy Craizy, Ally B na Tass.














WEMA SEPETU Afunguka Kuhusu Kutoka na Mkongo, Amechoka Kutumika Kama Daraja

Tangu mwaka 2016 uanze miongoni mwa story zilizochukua headlines kwenye mitandao mbalimbali ni hii inayomuhusu mwigizaji staa wa Tanzania, Wema Sepetu kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Mcongo.

Sasa leo kupitia instagram amejibu tetesi hizo na kuandika..‘Sijawahi na sitowahi kuwa na mwanaume Mcongo wa aina yoyote ile… Sasa nashangaa watu wameona mimi ndo daraja la kuwapa umaarufu… Im Tired… Huyo apocalypse sijui kitu gani aint my man… I only know him as a friend.So please guys niacheni kidogo tafadhal… Alam-siq…!!!🙏🏽🙏🏽🙏🏽 And ontop of all dat I think u all know me by now nikiwa na mtu sijivungi kumtangaza maana huwa I live to please my heart… Mwanaume wangu nadhani anajulikana’>> @wemasepetu

‘Sasa endeleeni kumpa huyo baba attention sababu yeye nako naona kashaona ni kamchezo kakupatia followers.Na nyie mnampa airtime ya kutosha anaendelea Ananiudhi na mimi kiukweli hadi napata hasira.But nakaa tu kimya… This is too much now’>>> wemasepetu
A photo posted by wemasepetu (@wemasepetu) on

Sunday, March 13, 2016

MAMA DIAMOND ATOBOA SIRI YA ZARI!

Mama Diamond  Sanura Kassim ‘Sandra’
 Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ametoboa siri ya mkaza mwanaye, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kushindwa kuishi Bongo na badala yake kukimbilia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Sandra au Mama D aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda juu ya uhusiano wake na Zari kufuatia tetesi kuwa hawaivi ndipo akaweka mambo sawa.
Mama D alisema kuwa yeye na Zari wapo vizuri lakini kinachomfanya mkwewe huyo kushindwa kuishi naye Bongo ni kutokana na biashara zake kudoda nchini Afrika Kusini.

“Unajua anapokuwa huku (Bongo), biashara zake huwa zinayumba sana, wakati mwingine akipiga simu akiulizia biashara zinakwendaje anaambiwa hali ni mbaya au hazijaingiza chochote hapo ndipo huwa anachanganyikiwa.
Diamond na mzazi mwenzake Zari.

“Kwa mfano hivi karibuni alipiga simu akaambiwa hakuna fedha kabisa na biashara haziendi. Kilichofuata ni kujiandaa na kumchukua Tiffah (Latifah Nasibu) kisha akaondoka zake.

“Hicho ndicho kinachomkimbiza Zari kuishi Bongo na si kweli kwamba hapapendi au kuna tatizo lolote,” alisema Mama D.

UKIACHANA NA YANGA, WAKIMATAIFA WENGINE HAWA HAPA KUTOKA EFM SPORTS

Baadhi ya watangazaji wa kipindi cha E Sport kinachorushwa hewani kupitia kituo cha EFM, Mauld Kitenge, Maestro na Oscar, wakiwa ndani ya studio za SuperSport nchini Africa Kusini tayari kwa kusongesha ajira mpya kupitia kipindi cha Swahili La liga. 
Maestro akiwa ndani ya studio za SuperSport zilizopo nchini Afrika Kusini na Mauld Kitenge ambapo wamekuwa wakienda kila mwisho wa juma kwaajili ya kurusha laivu matangazo ya kiswahili kupitia SuperSport Swahili La liga. Wamedhihilisha kuwa na wao ni wa kimataifa kutokea Tanzania hadi Swahili La liga World of champions.

SAMATTA AENDELEA KUCHANUA GENK,ATUPIA GORI LA KWANZA!



Mtanzania Mbwana Samatta amezidi kuonyesha makali baada ya kufunga bao lake la pili leo wakati KRC Genk ikishinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Oostende katika mechi ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.


Samatta amefunga bao la kwanza katika dakika ya 24 kwa kichwa likiwa ni la pili kwake tokea ajiunge na timu hiyo akitokea TP Mazembe ya DR Congo.

Leon Bailey alifunga la pili katika dakika ya 39 na kuifanya Genk kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani.



Kipindi cha pili wageni waliendelea kucharuka lakini Genk iliendelea kuwa makini na kuendelea kuondosha hatari.

Genk ilipata mabao mengine mawili lakini tayari Samatta alikuwa ametoka katika dakika ya 74 na Igor de Camargo akaingia kuchukua nafasi yake.

Alejandro Pozuelo aliifungia Genk bao la tatu katika dakika ya 81 na Igor aliyeingia kuchukua nafasi ya Samatta akafunga la nne katika dakika ya 88 kabla ya wageni Oostende kufunga la kufutia machozi katika dakika za majeruhi kupitia Sebastiani Siani.

MAGUFULI AMNG'ALISHA PAUL MAKONDA DAR ES SALAAM!


Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1.Mh. Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
2.Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga – Mkuu wa Mkoa wa Geita.
3.Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
4.Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
5.Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
6.Mh. Godfrey Zambi – Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
7.Dkt. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
8.Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
9.Mh. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
10.Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida.
11.Mh. Antony Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
12.Mh. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
13.Mh. Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
14.Mh. Jordan Mungire Rugimbana – Mkuu wa Mkoa Dodoma.
15.Mh. Said Meck Sadick – Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
16.Mh. Magesa Mulongo – Mkuu wa Mkoa Mara.
17.Mh. Amos Gabriel Makalla – Mkuu wa Mkoa Mbeya.
18.Mh. John Vianey Mongella – Mkuu wa Mkoa Mwanza.
19.Mh. Daudi Felix Ntibenda – Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
20.Mh. Amina Juma Masenza – Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
21.Mh. Joel Nkaya Bendera – Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
22.Mh. Halima Omary Dendegu – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
23.Dkt. Rehema Nchimbi – Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
24.Mhandisi Evarist Ndikilo – Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
25.Mh. Said Thabit Mwambungu – Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
26.Luteni Mstaafu Chiku Galawa – Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 2016

Friday, March 11, 2016

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA LULU, RICHIE KWA USHINDI WA TUZO MBILI!

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imefarijaka kwa ushindi wa wasanii wa filamu nchini walioshinda tuzo za filamu Afrika za mwaka 2016 (African Magic Viewers Choice Award) ziliyofanyika jijini Lagos nchini Nigeria mwishoni wa wiki iliyopita.


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imefarijaka kwa ushindi wa wasanii wa filamu nchini walioshinda tuzo za filamu Afrika za mwaka 2016(African Magic Viewers Choice Award) ziliyofanyika jijini Lagos nchini Nigeria mwishoni wa wiki iliyopita.

Waziri Mkuu Majaliwa, amesema hayo leo katika ukumbi wa mikutano ulipo katika Ofisi yake Jijini Dares Salaam, alipokutana na washindi wa tuzo za filamu Afrika za mwaka 2016 (AMVCA) ambao ni Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki na Single Mtambalike ‘Richie’ aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili pamoja Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Annastazia Wambura,Katibu Mkuu wa wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso na wasanii wa filamu.

“Serikali imefarijika sana kwa nyie kwenda Nigeria na kushinda na mmetumia lugha ya Kiswahili, lazima tutumie nafasi hii kuwatangaza pia mmuendelee na fani hii ili kuvutia wengi zaidi” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amewapongeza wasanii hao na kusema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wasanii wakati wowote na amewataka kujipanga vizuri kutumia vyama vyao vya sanaa na kusisitiza kuwa Mhe. Rais John Pombe Magufuli ametoa matamko kadhaa kuhusu sanaa na wasanii na ameendelea kushughulikia malalamiko yao ikiwemo suala la COSOTA, na kusema kuwa baada ya taratibu zote kukamilika suala hilo litasimamiwa na Wizara inayohusika na kazi za Sanaa.

Waziri Mkuu Majaliwa, pia amewataka watanzania kuacha tabia ya kutojiamini na kujidharau, na kuwataka watu waige mfano kwa wasanii hao, na kuwashauri wasanii wote kwa ujumla kutumia vyombo vya habari kujiimarisha na kujitangaza.

Kwa upande wao, wasanii waliopata tuzo hizo kwa filamu ya “mapenzi ya Mungu” ya Elizabeth Michael na filamu ya “Kitendawili” ya Single Mtambalike, wameishukuru Serikali kwa kuwathamini na kuonesha ushirikiano katika kazi zao za sanaa, na wameahidi kuendelea kutengeneza kazi nzuri za sanaa ili ziweze kuitangaza Tanzania kimataifa.

Naye, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Saimon Mwakifamba ameishukuru Serikali kwa jitihada mbalimbali inazofanya katika kusaidia tasnia ya sanaa kwa ujumla na ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza tasnia hiyo kimataifa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Tuzo kutoka kwa Msanii wa filamu Elizabeth Michael ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigearia. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akipokea tuzo kutoka kwa msanii wa filamu, Single Mtambalike ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigeria. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


NIYONZIMA AANIKA SIRI YA YANGA SC. KWA WANYARWANDA WENZAKE!

Kiungomachachali wa timu ya Yanga SC, Haruna Niyonzima.


KIUNGO nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima, ametoa onyo kwa Wanyarwanda kwamba Yanga iko mjini Kigali kuifunga APR.
Niyonzima ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, amewaambia waandishi wa habari mjini hapa, kwamba kilichowaleta mjini Kigali ni kuishinda APR.

Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi leo Kigali, Rwanda.
Kesho Jumamosi, Yanga itakuwa mgeni wa APR katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Amahoro jijini hapa. Akionyesha kujiamini, Niyonzima alisema Yanga imejiandaa vilivyo katika mechi hiyo na inataka ushindi.
“Hakuna asiyejua APR ni timu nzuri, lakini mjue Yanga imekuja Rwanda kwa ajili ya ushindi. Tunataka kushinda mechi ya kwanza.
“Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anataka kushinda. Hili mlijue,” alisema Niyonzima akionyesha kujiamini.
Niyonzima alijiunga na Yanga akitokea APR ambayo alikuwa mchezaji tegemeo wa kikosi hicho chini ya Kocha Ernie Brandts.
Mchezaji mwingine ambaye alijiunga Yanga akitokea APR alikuwa ni Mbuyu Twite ambaye asili yake ni DR Cingo.

LOWASSA AMTEMBELEA MAALIM SEIF SERENA HOTELI

Waziri Mkuu Mstaafu na Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati alipokwenda kumjulia hali katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akifanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati alipokwenda kumjulia hali katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2015.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya hali ya afya yake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, mara bade ya kumjulia hali katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo Machi 11, 2015

NAIBU WAZIRI WA KAZI, AJIRA NA VIJANA ATHONY MAVUNDE AZINDUA TAMTHILIA YA 'KELELE'

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (wa saba kutoka kushoto), akiwa kwenye pozi la pamoja na baadhi ya washiriki wa tamthilia hiyo.

NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, usiku wa kuamkia leo amefanikisha uzinduzi wa tamthilia mpya ya Kelele, iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza na Kukuza Vipaji (Tanzania House of Talent – THT).

Uzinduzi huo ulifanyika   ndani ya Ukumbi wa Paparazi uliopo katika Hoteli ya Slipway Masaki jijini Dar es Salaam.  Akizungumza muda mfupi kabla ya kuzindua tamthilia hiyo. Mavunde alisema kwamba, anawapongeza  THT kwa kuendelea kuisaidia serikali kwenye suala la kuwatafutia vijana ajira.

“Tunaishukuru sana THT kwa kuendelea kuiunga mkono serikali kwenye suala la kutatua na kuendelea kuongeza ajira kwa vijana wetu, tunatambua wazi kabisa kuwa serikali pekee haiwezi kumaliza tatizo hili pasipo watu binafsi kuongeza ajira kwa namna hii,” alisema Mavunde.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa THT, Ruge Mtahaba, alimpongeza Mavunde  kwa kuitikia wito wa kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa filamu hiyo.
Mavunde akiongea jambo wakati wa uzinduzi huo ukumbi wa Paparazi Masaki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa THT, Ruge Mtahaba, akielezea namna walivyoiandaa tamthilia hiyo.
Baadhi ya wanamitindo wakitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Msanii wa Hip Hop, Farid Kubanda ‘Fid-Q’ (katikati), akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchovu na Mtangazaji wa East Africa Radio, Ana Peter.
Baadi ya waimbaji wa THT Band wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo.

Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo, Nahreel na Aika wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Wanamitindo wakiwa katika pozi la pamoja baada ya kumaliza kutoa burudani.
Warembo wakiwa mbele ya kamera.
Mwana mitindo maarufu Bongo, Ally Rehmtulah, akiwa  na mrembo.
Mtangazaji wa Clouds TV, Shadee akiwa kwenye pozi kwenye Red Carpet.
Mtangazaji wa Clouds FM na TV, Hamisi Dakota.
Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchovu na rafikiye.
Vijana wanauonda kundi la Makomando wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo wakibadilishana mawazo.


POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...