|
Naibu Waziri wa
Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (wa saba kutoka kushoto), akiwa kwenye
pozi la pamoja na baadhi ya washiriki wa tamthilia hiyo.
|
NAIBU Waziri wa
Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, usiku wa kuamkia leo amefanikisha
uzinduzi wa tamthilia mpya ya Kelele, iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza na
Kukuza Vipaji (Tanzania House of Talent – THT).
Uzinduzi huo
ulifanyika ndani ya Ukumbi wa Paparazi uliopo katika Hoteli
ya Slipway Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuzindua tamthilia hiyo. Mavunde alisema
kwamba, anawapongeza THT kwa kuendelea
kuisaidia serikali kwenye suala la kuwatafutia vijana ajira.
“Tunaishukuru
sana THT kwa kuendelea kuiunga mkono serikali kwenye suala la kutatua na
kuendelea kuongeza ajira kwa vijana wetu, tunatambua wazi kabisa kuwa serikali
pekee haiwezi kumaliza tatizo hili pasipo watu binafsi kuongeza ajira kwa namna
hii,” alisema Mavunde.
Kwa upande wa
Mkurugenzi Mkuu wa THT, Ruge Mtahaba, alimpongeza Mavunde kwa kuitikia wito wa kuwa mgeni rasmi wa
uzinduzi wa filamu hiyo.
|
Mavunde
akiongea jambo wakati wa uzinduzi huo ukumbi wa Paparazi Masaki jijini Dar es
Salaam.
|
|
Mkurugenzi
Mkuu wa THT, Ruge Mtahaba, akielezea namna walivyoiandaa tamthilia hiyo. |
|
Baadhi ya wanamitindo
wakitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
|
|
Msanii
wa Hip Hop, Farid Kubanda ‘Fid-Q’ (katikati), akibadilishana mawazo na
Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchovu na Mtangazaji wa East Africa Radio, Ana
Peter. |
|
Baadi ya
waimbaji wa THT Band wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
|
|
Wasanii
wanaounda kundi la Navy Kenzo, Nahreel na Aika wakifuatilia kwa makini uzinduzi
huo.
|
|
Wanamitindo
wakiwa katika pozi la pamoja baada ya kumaliza kutoa burudani.
|
|
Warembo wakiwa mbele
ya kamera.
|
|
Mwana
mitindo maarufu Bongo, Ally Rehmtulah, akiwa na mrembo. |
|
Mtangazaji wa
Clouds TV, Shadee akiwa kwenye pozi kwenye Red Carpet.
|
|
Mtangazaji wa
Clouds FM na TV, Hamisi Dakota.
|
|
Mtangazaji
wa Clouds FM, Adam Mchovu na rafikiye. |
|
Vijana
wanauonda kundi la Makomando wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo. |
|
Baadhi ya
wadau waliohudhuria uzinduzi huo wakibadilishana mawazo.
|
No comments:
Post a Comment