Friday, March 11, 2016

NIYONZIMA AANIKA SIRI YA YANGA SC. KWA WANYARWANDA WENZAKE!

Kiungomachachali wa timu ya Yanga SC, Haruna Niyonzima.


KIUNGO nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima, ametoa onyo kwa Wanyarwanda kwamba Yanga iko mjini Kigali kuifunga APR.
Niyonzima ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, amewaambia waandishi wa habari mjini hapa, kwamba kilichowaleta mjini Kigali ni kuishinda APR.

Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi leo Kigali, Rwanda.
Kesho Jumamosi, Yanga itakuwa mgeni wa APR katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Amahoro jijini hapa. Akionyesha kujiamini, Niyonzima alisema Yanga imejiandaa vilivyo katika mechi hiyo na inataka ushindi.
“Hakuna asiyejua APR ni timu nzuri, lakini mjue Yanga imekuja Rwanda kwa ajili ya ushindi. Tunataka kushinda mechi ya kwanza.
“Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anataka kushinda. Hili mlijue,” alisema Niyonzima akionyesha kujiamini.
Niyonzima alijiunga na Yanga akitokea APR ambayo alikuwa mchezaji tegemeo wa kikosi hicho chini ya Kocha Ernie Brandts.
Mchezaji mwingine ambaye alijiunga Yanga akitokea APR alikuwa ni Mbuyu Twite ambaye asili yake ni DR Cingo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...