Kwa mujibu wa Mkwe wa marehemu, Wema Mustapha
Mgombelwa 'Baba Wawili" shughuli za mazishi ya marehemu Mzee Mapili
zitafanyika Magomeni Mapipa Mtaa wa Magomeni Namba 21.
Wema
alisema: "Tunaweza kumzika katika makaburi ya Mwinyimkuu au Kisutu jijini
Dar es Salaam leo (Ijumaa),."
Mkwe huyo
ambaye ni seneta maarufu wa Bendi ya Msondo Ngoma alisema mkwe wake alifariki
Jumanne usiku baada ya kutoka kuangalia mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya
Arsenal na Barcelona.
"Kikubwa
alikuwa akisumbuliwa na presha kwa muda mrefu, alifariki usiku na maiti yake imepelekwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Baada ya
kupata taarifa za msiba huo tunawaomba ndugu jamaa na marafiki kujumuika pamoja
katika mazishi ya kumhifadhi mzee wetu," alisema Wema.
|
No comments:
Post a Comment