Sunday, October 18, 2015

Baadhi ya wachezaji wa Simba SC, wakishangilia goli lao baada ya kuichapa Mbeya City.

SIMBA Sports Club ya jijini Dar es Salaam, jana imevunja mwiko wa kufungwa na kutoa droo na timu ya Mbeya City baada ya kuwafunga goli moja kwa sifuri katika dimba la Sokoine, ushindi ambao ni historia kwao kutokana na kuteswa na wanakomakumwanya hao kwa mda wa misimu miwili iliyopita.

Histori ya wagonga nyundo  imevunjwa na  Simba kwa goli moja tu maridadi lililowekwa nyavuni na Mganda wa timu hiyo Juuko Murushidi dakika ya pili ya mchezo, goli ambalo katika ligi kuu msmu huu litakuwa la  mapema zaidi katika uwanja huu ukiachia mbal goli la Atupele Green wa Ndanda FC,  liliofungwa dakika ya 3.

Kikosi cha Simba SC, na Mbeya City kikipambana kabla ya Juuko kupachika bao.
Wachezaji wa Simba SC, Mussa Hassani Mgosi na Juuko Murushidi wakishangilia baada ya kuifunga Mbeya City.

Staili ya ushangiliaji ya ina yake iliyoonyeshwa na wachezaji wa Simba.
..wakishangilia kwa pamoja.
Mabosi wa timu ya Simba wakifurahia jambo uwanjani hapo.
Mmoja wa mashabiki wa  Mbeya City akiwa amebebwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu kwenye mchezo huo.No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...