Sunday, June 28, 2015

KANYE WEST AFANYA KWELI TAMASHA LA GLASTONBURY, AVAMIWA NA NJEMBA STEJINI

Kanye West akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria Tamasha la Glastonbury nchini England jana usiku.

Komediani wa Uingereza, Lee Nelson baada ya kupanda stejini kumpa sapoti Kanye West.
RAPPA wa nchini Marekani, Kanye West amefanya kweli kwa kuangusha bonge la shoo katika Tamasha la Glastonbury nchini England jana usiku.


Mashabiki wakifuatilia burudani kutoka kwa Kanye West.
Mkali huyo alizikonga vilivyo nyoyo za mashabiki mbali na watu zaidi ya 134,000 kupinga uteuzi wa jina lake kuwemo kwenye orodha ya watu waliopanga kutumbuiza katika tamasha hilo wakitaka aondolewe na iwekwe Bendi ya Muziki wa Rock huku mwandaaji wa tamasha hilo, Emily Eavis akipokea vitisho vya kuuawa kupitia Twitter kwa uamuzi wa kumualika West.

Kanye akizidi kufanya yake.

Mke wa Kanye, Kim Kardashian akichukua picha wakati mumewe akiwa stejini.
Shoo hiyo ya West, iliingiliwa na komediani raia wa Uingereza aitwaye Lee Nelson aliyepanda stejini kumpa sapoti staa huyo kabla ya kushushwa na wanausalama.

Kanye na Kim wakati wakiwasili Glastonbury tayari kwa shoo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...