Monday, March 2, 2015

UCHAMBUZI WA KINA JUU YA MECHI YA SIMBA NA YANGA

# Ukizubaa umeliwa siku hiyo
# Timu zote zalihama jiji kwa muda


Wakati homa ya mtanange wa mahasimu, Simba na Yanga likizidi kushika kasi, timu hizo zimeamua kuondoka jijini Dar na kwenda kuweka kambi mbali kabisa katika kujiandaa na mchezo huo.
Timu hizi zenye historia kubwa katika soka la Tanzania, zinatarajiwa kukutana Machi 8, mwaka huu- yaani Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa.
Simba wao wameweka kambi kisiwani Zanzibar ambapo aliondoka jana mchana huku Yanga wao wakiindea Bagamoyo, windo ambalo limekuwa na matokeo mazuri kwao.
Mchezo huo unatajwa kuwa na msisimko wa aina yake kutokana na timu hizo kuwa na rekodi zao. Katika mechi tano za mwisho timu hizo kukutana, Simba imekuwa na rekodi nzuri, ambapo imeshinda mechi mbili; kwenye Nani Mtani Jembe huku kwenye ligi zikitoka sare katika mechi tatu walizokutana.

Msimu uliopita, timu hizo zilitoshana nguvu kwa matokeo ya 3-3 katika raundi ya kwanza, kabla ya kutoka 1-1 katika mzunguko wa pili. Msimu huu, raundi ya kwanza zilitoka suluhu.

Hata hivyo, bado hiyo si sababu ya kuhukumu mchezo wa wikiendi hii kwani Yanga chini ya Hans Pluijm kwa sasa ni mwendo wa kuvunja rekodi zilizoshindikana.

Alianza na ushindi kwenye Uwanja wa Jamhuri ukiwa ni wa kwanza baada ya miaka sita wakati Yanga ilipoichapa Polisi bao 1-0 hivi karibuni, kabla ya kuandikisha rekodi mbili tofauti kwenye Dimba la Sokoine Mbeya. Moja ya kufunga mabao mengi zaidi uwanjani hapo-mabao 6-1 kwa kuzichapa Mbeya City na Prisons mabao 3-1 na 3-0. Pili, ulikuwa ushindi wa kwanza wa Yanga baada ya miaka sita kupita.

Simba wao wanajivunia kuendeleza rekodi, licha ya kwamba Yanga imekuwa ikionekana kuwa nzuri zaidi ya Simba muda mrefu, lakini kila wakikutana uwanjani, mambo huwa tofauti.

Simba inaingia ikiwa na rekodi ya kuwa timu ya kwanza msimu huu kufunga mabao mengi katika mechi moja kwenye Uwanja wa Taifa, lakini pia ikijivunia rekodi ya kuinyanyasa Yanga msimu wa pili sasa.



Watu wa kuchungwa
Simba: Nguvu yao ipo kwa kiungo Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu kutokana na kiwango chao kwa sasa, lakini watu kama Emmanuel Okwi, Elias Maguri na Awadhi Juma wamekuwa watu wasumbufu sana kila wanapokutana na Yanga.
Yanga: Mrisho Ngassa, Simon Msuva pamojana mabeki, Kelvin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambao wamekuwa ‘waki-perfom’ sana katika mechi za mahasimu. Lakini Amiss Tambwe ana nafasi kubwa ya kuwafunga Simba, atakuwa akitaka kulipa kisasi cha kuachwa bila sababu za msingi zilizotajwa.

Lakini hasira zaidi zipo kutaka kuwakomesha kutokana na kudhurumiwa hela zake, huku akiwa kwenye mchakato wa kuwashitaki kutokana na danadana anazopigwa siku hadi siku.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...