Thursday, March 5, 2015

MAIMARTHA : NIKIWA CHUMBANI HUWA SIVAI NGUO ZAIDI YA CHENI NA VIKUKU TU!


Wiki hii kupitia safu hii tunaye Maimartha Jesse ‘Mai’ ambaye ni mtangazaji na mjasiriamali. Mwandishi wetu Hamida Hassan alimbana kwa maswali 10 mengi yakiwa yanahusu mambo ya chumbani zaidi, ungana naye…

TQ: Ni chakula gani kizuri ambacho ukimpikia mumeo anasikia raha?

Mai: Mume wangu ni mpenzi sana wa wali samaki au ugali samaki, sambamba na vikorombwezo vingine.

TQ: Ukiwa sebuleni na mumeo mkiangalia vipindi mbalimbali vya televisheni ni mavazi gani unavaa na mapozi gani mnakaa?

Mtangazaji wa B&M, Maimartha Jesse.

Mai: Huwa tunakaa kwa heshima tu kwa sababu nina familia na wakati wote inakuwa karibu yetu.

TQ: Vipi uwapo chumbani na mumeo unapendelea kumtega kwa mavazi gani au nakshi zipi?

Mai: Kiukweli kule hakuna kuvaa nguo, ni cheni ya kiunoni, vikuku mguuni kwani tunakuwa wawili tu. Si unajua tena pale ndiyo eneo la kujidai na laazizi wangu?

TQ: Kwa mapenzi hayo mnayooneshana, siku ikitokea umemfumania mumeo na mwanamke mzuri kuliko wewe, utachukua uamuzi gani?

Mai: Siwezi kumuacha mume wangu kwa sababu jiji hili lina wanawake wabaya ambao wanajipeleka wao kwa wanaume. Nitakachokifanya ni kumvalisha mume wangu nguo kisha namrudisha nyumbani. Nikifika namuandalia juisi bariiidi. Baada ya hapo nitaenda kumalizana na mwizi wangu.

TQ: Utamfanya nini huyo mwizi wako?

Mai: Ukweli ajiandae kwa viwembe kwani nitahakikisha nimemchakaza sura yake, akitoka hapo akiona mume wa mtu atamuogopa kama ukoma.

TQ: Inasemekana una hausigeli mkali sana, vipi siku mumeo uzalendo ukimshinda na ukawakuta kwenye kitanda mnacholala?

Mai: Hilo haliwezi kutokea. Unajua nimeshamsoma mume wangu na kugundua hawezi kujivunjia heshima yake kwa kutembea na mfanyakazi wetu, ila siku ikitokea ndiyo nitajua cha kufanya.

TQ: Kuna haka kaskendo ka’ mastaa wengi kujihusisha na usagaji? Wewe umeshawahi kushiriki kwa namna yoyote?

Mai: Huo ni uchafu, anayefanya hivyo maisha yamemshinda, hutasikia hata siku moja mimi nimefanya ujinga huo.

TQ: Inadaiwa wewe kwa kuchepuka ni noma na una kidumu chako (mwanaume wa pembeni), taarifa hizi zina ukweli wowote?

Mai: Heshima niliyonayo kwa kuitwa mke wa mtu siwezi kuitia doa, najiheshimu sana kuliko watu wanavyofikiria. Huwezi kuamini mimi nawashangaa sana wanaochepuka.

TQ: Kabla ya ndoa umewahi kutoka na wanaume wangapi?

Mai: Kiukweli idadi ipo ila sipendi kuitaja kwa kuwa nahisi nitamkwaza mume wangu .

TQ: Kuna madai kuwa shepu uliyonayo Mchina anahusika sana, hebu funguka.

Mai: Hayo ni mambo yangu binafsi sipendi kuyaongelea bwana, kila mmoja ana maisha yake aliyoyachagua.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...