Thursday, March 5, 2015

ANGALIA PICHA ZA WATU, MIFUGO MAAJABU YALIYOTOKEA KATIKA MVUA KUBWA ILIYONYESHA MKOANI SHINYANGA

 
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua huko Kahama imefikia watu 42 wengi wakiwa ni watoto huku majeruhi waliofikishwa hospitali wakiwa ni 91.
Watu 35 walifariki dunia papo hapo na wengine wakiwa hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo na mawe yanayodariwa kuwa na ukubwa mithili ya ndoo ndogo ya lita 10 katika kijiji na Kata ya Mwakata wilayani Kahama, mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia jana.
Malunde1 blog imeambiwa kuwa mvua hiyo imenyesha kwa muda wa takribani dakika 30,imeua pia mifugo wakiwemo ng’ombe na mbuzi na kuharibu vibaya mimea. 
 Afisa mtendaji wa kata ya Mwakata Mahega Mwelemi ameiambia Malunde1 blog kuwa maeneo yaliyoathirika kuwa ni cha Mwakata,Nhumbi na Magung’humwa.
  ANGALIA PICHA



Magari yakielekea kwenye kata ya Mwakata wilayani Kahama kwa ajili ya uokoaji na kutoa misaada zaidi kwa wahanga wa tukio hilo.Picha zote na Faraji Mfinanga,Shabani Alley na Mohab Dominic-Malunde1 blog Kahama

Mwananchi akiwa amebeba moja ya barafu la mvua,yaliyokuwa yanadondoshwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.



Watu 38 wamefariki dunia na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mwakata Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 



Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya(mwenye suti) amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.


Viongozi wakiwa eneo la tukio

Barafu maarufu MAWE ikiwa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika







 


 
PICHA, HABARI KWA HISANI YA MALUNDE BLOG, KAHAMA. 

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...