Friday, March 6, 2015

CHID BENZ AJIPELEKA KWA SNURA



Mkali wa Vokal za kigumu hapa Bongo, Chid Benz ametajwa katika kuhusika katika track mpya ya Mamaa Majanga, Snura ambayo inasumbua sokoni kwa sasa, inayokwenda kwa jina la Hawashi, aliyomshirkisha Nay wa Mitego.
Snura ndiye aliyemwaga data zote leo wakati akifanya mahojiano na Globaltv Online kuhusu ngoma yake yenye mahadhi ya Hip Hop, ambapo alisema ni matunda ya Chid Benz aliyempa mistari ya kuimba baada ya kumkuta studio akitaka kurekodi ngoma nyingine, hivyo kuamua kuachana na mistari yake na kurekodi ile aliyopewa na Chid.
Chid Benz
Alifunguka kuwa Chid alitinga studioni hapo na kumkuta Mamaa Majanga kisha kumweleza meneja wake (HK) kwamba Snura asingetoka kwa ngoma aliyokuwa akirekodi baada ya kimya kirefu kupita.
“Nilikuwa studio narekodi, mara akaja Chid kisha kumweleza meneja wangu kuwa nisingetoka kwa ngoma niliyokuwa narekodi. Akasema kuwa atanipa mistari ya kuimba na ni lazima nitoke. Basi, alinipatia mistari hiyo na nikairekodi kisha kuiingiza soka na sasa ngoma iko sokoni,” anasema Snura.
Kwa mahojiano zaidi, tembelea Global TV Online

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...