Saturday, February 14, 2015

TAMBWE AZALIWA UPYA TAIFA, ATUPIA ZOTE YANGA IKIBOMOA NGOME YA WANAJESHI WA BOTSWANA

Tambweeee..... Nyota wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe akishangilia bao lake la kwanza na kocha wake, Hans van Der Pluijm leo Taifa.

Wachezaji wa Yanga wakimkumbatia kocha wao, Pluijm wakishangilia bao la kwanza dhidi ya BDF.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto akimkabiri fowadi wa BDF Vicent Nzombe.
Ikiwa ni mechi yake ya kwanza kucheza michuano ya kimataifa akiwa kwenye adhi ya Tanzania, Straika Mrundi, Amissi Tambwe leo amekuwa nyota wa mchezlo baada ya kuibeba Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya BDF XI ya Botswana.
Katika mchezo huo wa kombe la shirikishisho Afrika mchezo wa raundi ya kwanza hatua ya awali, Tambwe alitumbukia nyavuni mara mbili katika dakika ya kwanza akiunganishwa kwa kichwa mpira wa Haruna Niyonzima, aliyepenyeza krosi ya kona ndogo iliyoanzishwa na Simon Msuva.
Yanga ilikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengi kipindi cha kwanza kutokana na mfumo wa wapinzani wao kucheza soka la kujilinda zaidi tangu ya mwanzo wa mchezo, lakini mafowadi hawakuwa makini na lango.
Hadi mapumziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa bao moja. Tambwe aliwanyayua vitini mashabiki wa Yanga tena katika dakika ya 55 baada ya kumalizia krosi murua iliyochongwa na Mrisho Ngassa.
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema kuwa anafurahia ushindi huo, japo aliingia uwanjani akihitaji mabao mengi lakini hata hayo mawili ni hazina nzuri kwao na kuahidi kucheza kwa tahadhari ya juu katika mchezo wa marudiano.
Kocha wa BDF, Letang Kgengwenyane alisema hakuwa na cha kusema zaidi ya kusifia kiwango kizuri kilichoonyeshwa na Yanga na kukubali kichapo hicho, lakini akahidi kujirekebisha na kuhakikisha wanalipiza kisasi kwenye mchezo wa amrudiano utakaopigwa Februari 27 mjini Gabrone, Botswana.
Hii ni mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa Tanzania, baada ya kujiunga na Yanga akitokea Simba ambayo aliachana nayo msimu uliopita. Simba haijashiriki michuano ya kimataifa, msimu wa pili mfululizo, ambapo msimu ulioopita ilimaliza nafasi ya nne.
Penalti??? No.. beki wa Yanga, Mbuyu Twite kushoto akionekana kumfanyia madhambi fowadi wa BDF Kabelo Seakanyeng lakini mwamuzi, Thiery Nkurunziza hakuamua chochote.
 
  

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...