Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakimhoji binti aliyejitambulisha kwa jina la Coletha akisadikika kuwa mchawi..soma chini kwa kina. |
Ikiwa ni wiki 2 tu zimepita baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi (80) kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi hajitambui katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembeza mjini Shinyanga,matukio yanayohusishwa na imani za kishirikina yameendelea kuacha watu midomo wazi ambapo leo asubuhi binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 aliyedaiwa kuwa mchawi amekutwa hajitambui akiwa amevaa nguo nyeusi,kashikilia chungu kidogo kwenye mlango wa nyumba ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga huku akidai kuwa amefika mahali hapo kwa kutumia chungu-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga.
Tukio hili limetokea leo asubuhi katika mtaa wa Bushushu nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake zaidi ya 10 kutoka kanda ya ziwa kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe ili ndugu yao aolewe na baba wa familia hiyo.Kwa mujibu wa ndugu wa baba mwenye nyumba wameiambia Malunde1 blog kuwa kweli ndoa hiyo ilivunjika tangu tarehe 17.9.2014
Pichani binti aliyejitambulisha kwa jina la Coletha akiwa amevaa kishirikina huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai kuwa alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 Geita,Mwanza na Shinyanga kuwanga katika nyumba hiyo.Baada ya kukutwa hapo mlangoni wakazi wa eneo hilo walifika eneo la tukio kisha mwenyekiti wa mtaa huo Ruben Masanja akimwomba mwenye nyumba amruhusu binti aingie ndani kwa usalama wake.
Binti huyo amesema leo ni mara ya tatu wanakuja kufanya uchawi wao,lengo lao ni kutaka ndugu yao aolewe na Massawe,walikuja siku ya kwanza wakakuta mke wa Massawe akisali, wakashindwa,wakarudi kwa mara ya pili kwa ajili ya kusambaratisha ndoa,wakafanikiwa, leo yeye alikuwa kiongozi wa wachawi wengine walikuja kufanya sherehe kwa kazi nzuri waliyoifanya lakini wenzake wamemkimbia.

Wakazi wa Shinyanga wakichungulia kwenye madirisha kuona kinachoendelea ndani.
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wakimhoji binti huyo.
ambapo baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga wakitumia vyungu na ungo majira ya saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary Joseph.
Askari polisi kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wanaotumia pikipiki kuzunguka maeneo mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga wakijadili jambo ndani ya nyumba alimohifadhiwa binti huyo
Askari polisi wakimlinda Binti huyo asipigwe na wananchi waliofika eneo la tukio.
Binti akiondolewa eneo la tukio.
Binti akiwa ndani ya gari la polisi. Gari la polisi likiondoka eneo la tukio. Wakazi wa Shinyanga wakiondoka eneo la tukio-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga.
STORI& PICHA KWA HISANI YA MALUNDE1 BLOGU.
No comments:
Post a Comment