Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Azam pamoja
na mabingwa wa kihistoria wa Kombe la Kagame, Simba zimelazimishwa sare hivyo
kujiweka pabaya katika mbio za kuwania ubingwa ambapo wameishusha Yanga presha
ya kujikita kileleni.
![]() |
Kiungo wa Simba, Abdi Banda katikati akiwatoka wachezaji wa Coastal Union. Kushoto ni kiungo wa zamani wa Simba, Abdulhalim Humud. |
Azam imelazimishwa mabao 2-2 na Polisi Moro
kwenye Uwanja wa Jamhuri, ambapo mabao ya Azam yakifungwa na mapacha, Kipre
Tchetche na Kipre Balou. Mabao ya Polisi yemefungwa na Said Bahanuzi na Kassim
Selembe.
Matokeo hayo ni kwamba Azam anafikisha
pointi 22, sawa na Yanga lakini wao watashuka dimbani kesho kumenyana na Mtibwa
kwenye Uwanja wa Taifa.
Katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba
imeendelea kuandamwa na matokeo ya sare, baada ya kulazimishwa suluhu na Wagosi
wa Kaya, huku Simba wakipoteza nafasi kadhaa kupitia kwa Elias Maguri, Danny Sserunkuma.
Matokeo hayo yameibakiza Simba na pointi
17, moja nyuma ya Coastal.
![]() |
Danny Ssernkuma wa Simba (kulia) katika harakati za kusaka bao mbele ya beki na kipa wa Coastal. |
Katika kile kilichoonekana wikiendi hii ni
mwendo wa sare, napo kwenye Uwanja wa Chamazi, Maafande wa JKT Ruvu walibanwa
mbavu na Mbeya City kwa kutoka sare ya bao 1-1. Wafungaji wakiwa ni Ally Bilal
kwa upande wa JKT huku Kenny Ally akiifungia City.
Nagwanda Sijaona, wenyeji Ndanda wamebanwa
mbavu na Stand kwa kutoshana nguvu ya bao 1-1 huku matokeo kama hayo pia
yakipatikana kwa Prisons na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
No comments:
Post a Comment