Sijui kosa langu...Fowadi wa zamani wa Juve, Giovinco ameamua kuikimbia nchi ya Italia, baada ya kuchoshwa na maisha ya kipweke! Hapendwi |
Straika wa Kiitalia, ambaye amejiunga na
klabu ya Toronto ya huko Canada, Sebastian Giovinco ametoa kali ya mwaka baada
ya kuweka bayana kuwa aliamua kuondoka nchini kwao, kutokana na kutopendwa na wengi.
Nyota huyo, 28, aliyejiunga na Toronto
akitokea Juventus ameonekana kuwa alikuwa hana mahusiano mazuri na kila mtu,
kuanzia vyombo vya habari hadi makocha waliopata kuifundisha Juve, akiwemo Antonio
Conte, Massimiliano Allegri na Cesare
Prandelli.
Akizungumza kwa mara ya kwanza katika
vyombo vya habari, muda mfupi baada ya kutua Canada, tayari kuungana na timu
yake mpya, Giovinco alifunguka kuwa alilazimika kuondoka
Juve baada ya kuchoshwa na kujiuliza juu ya uwezo wake wa sasa.
"Pale Italia nilikuwa na matatizo
mengi sana. Kila siku hakuna kingine cha kusema zaidi ya kujadili kiwango
changu kwamba siwezi kucheza katika kiwango cha juu, lakini nilikuwa nikipinga
katika hilo kila siku tena kwa hoja," alisema Giovinco.
"Nilitamani nitafute mji ama timu
ambayo ingenikaribisha vizuri, kama hii ilivyonipokea. Kwa hiyo ujio wangu huku
ulikuwa sahihi."
Lakini pamoja na hoja yake na shutuma kwa
maelewano mabaya na makocha wake pamoja na media kwa kulia kuwa hakupewa muda
wa kucheza, lakini takwimu zinakinzana na maneno yake kwani.
Katika msimu wa 2012/13 nyota huyo alipewa
nafasi mara 31 kwenye ligi kuu na kufunga mabao saba tu wakati kikosi chake kikitwaa ubingwa wa ligi
hiyo maarufu kama Serie A, ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.
Msimu uliopita 2013/14 alicheza mechi 17
za Serie A, zikiwemo sita akianza na akafunga mabao mawili tu, huku msimu huu
amezidi ‘kuharibu’ kwani amecheza mechi saba
na kuanza mechi mbili na hajafunga bao lolote.
No comments:
Post a Comment