Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni taarifa
za kurejea kwa mlinzi wa kati, Mganda, Joseph Owino ambaye anatarajia kurejea
kikosini mwezi huu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba,
Humprey Nyasio amesema nyota huyo wa zamani wa Azam, amekuwa akisumbuliwa na
jeraha za nyama za paja, lakini taarifa za kitatibu zinadai atakuwa fiti
kuanzia mwezi ujao-Februari.
Safu ya ulinzi ya timu hiyo imeonekana
kupwaya hivi karibuni kwa kuruhusu mabao mepesi, hali ambayo
Akizungumza na blogu hii, Nyasio alisema:
“Owino bado hajapona vizuri lakini kwa mujibu wa daktari, tutakuwa naye kuanzia mwezi ujao,” alisema Nyasio.
“Owino bado hajapona vizuri lakini kwa mujibu wa daktari, tutakuwa naye kuanzia mwezi ujao,” alisema Nyasio.
Safu ya kati ya ulinzi ya timu hiyo kwa
sasa inasimamiwa na nahodha Hassan Isihaka na Mganda, Juuko Murshid.
No comments:
Post a Comment