Nimerudi... Kiungo staa, Ndemla akipiga tizi la pekee leo katika mazoezi ya kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Moro, Jumamosi, wiki hii. |
Nyota aliye kunako kiwango cha kimataifa, Said Hamis Ndemla
ameanza rasmi mazoezi na timu hiyo, baada ya kuwa nje akisumbuliwa na jeraha. Katika
mazoezi ya kikosi hicho yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jeshi wa Mbweni, nje
kidogo ya jiji kinda huyo alipewa programu maalum ya kufanya mazoezi ya peke
yake akiwa chini ya uwangalizi wa daktari, Yassin Gembe.
Naye nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Joseph Owino amezidi
kuonekana fiti baada ya kufanya mavituzi ya ukweli katika mazoezi ya leo na
kuonekana kupona kabisa.
Ancle is back... Joseph Owino (wa pili kulia) amezidi kuonyesha kiwango kizuri baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua. |
No comments:
Post a Comment