Monday, February 9, 2015

DAKIKA 60 ZA KIFO SIMBA JESHINI HATAREEE TUPU!!!

Tizi kwa kwenda mbele katika Uwanja wa Mbweni jeshini jioni ya leo.

Twaha na 'ngeli' wapi na lini jamani.!!.. Kocha Goran Kopunovic (wa nne kutoka kushoto) akizungumza jambo na straika Ibrahim Twaha 'Messi wa Tanga'

Twaha Ibrahim 'Mess wa Tanga' akiwania mpira na Ramadhan Kessy katika mazoezi ya leo.
 
Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi ya kufa mtu katika Uwanja wa Mbweni nje ya kidogo ya jiji, ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa ‘kufa kupona’ ilmradi kupata pointi tatu muhimu, ambapo watakutana na Polisi Moro, mchezo utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa ‘gundu’, Jamhuri, Morogoro.
Uwanja huo umekuwa na historia mbaya kwa timu za Simba na Yanga, lakini Yanga tayari wamefanikiwa kuondoka mkosi huo, kwani wiki kadhaa zilizopita waliifunga Polisi bao 1-0.
Hata hivyo timu hiyo imezidi kupandwa na presha kutokana na nafasi isiyoridha ilipo kwa sasa, ikiwa katika nafasi ya 9 na alama 17 hivyo kusaka ushindi wa lazima Jumamosi ili kurejesha imani kwa mashabiki wake. Polisi Moro wao wakiwa kwenye nafasi ya 3 na pointi 19.
Katika kukamilisha hilo, mabingwa hao wa kihistoria wa kombe la Kagame na Mapinduzi, leo wameanza mazoezi rasmi kwenye Uwanja wa Jeshi, Mbweni ambapo kocha Goran Kopunovic alitumia ‘lisaa limoja’ tu kuwahenyesha wachezaji wake.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...