Messi, mchezaji bora wa rekodi wa dunia, ndiye kila kitu pale Barcelona.
Kun ndiye tegemeo la Man City tangu ajiunge na kikosi hicho mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid ya Hispania.
Kiungo na beki kiraka wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Javier Mascherano amewaonya watu kuhusu mijadala wanayoiweka kuhusu viwango vya wanasoka hatari kwa sasa, Sergio Kun Aguero na Lionel Messi, kuelekea mchezo utakapowakutanisha wawili hao wiki ijayo.
Kun ambaye ni jicho la Manchester City kwa sasa kama ilivyo Barcelona na Messi, watakutana katika mtifuano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini jicho la kila mtu liko kwa Kun na Messi.
"Agüero na Messi ni wachezaji wenye vipaji wa hali ya juu. 'Kun' ni mchezaji wa aina yake, ni mtu hatari karika kusaka bao na anaweza kupenya hata kwenye msitu wa mabeki, ni mtu hatari wa aina yake. Ila ni vigumu sana kumlinganisha na Messi, sababu Messi ni bora na hakuna wa kufikia levo ya kiwango chake", alisema Muargentina mwenzao, Mascherano.
Hata hivyo anaamini bado wana nafasi kubwa ya kupata ushindi katika mchezo huo utakaopigwa Jumanne wiki ijayo, lakini mechi hiyo itakuwa pasua kichwa.
"City watakuwa wakitazamania mengi kwenye michuano hii, sababu ndio michuano mikubwa kwao na wanajaribu kukua zaidi mwaka hadi mwaka kwenye michuano hii. Zitakuwa ni mechi mbili ngumu kuliko maoenezo, sababu sisi (Barca) ndio timu pinzani katika ukanda wa Ulaya".
Mjue kutofautisha ndizi na tango... Mascherano ameonya wanaowalinganisha Kun na Messi. |
Messi kulia na Kun Aguero katia moja ya mazoezi kwenye kikosi cha timu ya taifa, Argentina. |
No comments:
Post a Comment