Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe akiwa ameanguka muda mfupi baada ya kukosea ngazi alipokuwa akishuka tayari kwa kuingia kwenye gari lake kwenye Uwanja wa Ndege wa nchi hiyo alipokuwa akitokea nchini Ethiopia.
HATIMAYE picha zinazoonyesha tukio la kudondoka kwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 90, zimezidi kusambaa kwa kasi huku baadhi ya watu wanaojua kucheza na teknolojia wakizibadili na kulifanya tukio kama la utani.
Ukweli wa tukio hilo ulikuwa hivi, Mh. Mugabe alidondoka Ijumaa iliyopita katika Uwanja wa Ndege wa Nchi hiyo, muda mfupi tu bada ya kukosea kukanyaga moja ya ngazi ya jukwaa alilokuwa akiongelea, mara baada ya kutua hapo akitokea nchini eiThiopia ambako alienda kwaajili ya shughuli zake za kiserikali.
No comments:
Post a Comment