Moja ya picha katika tukio lililosababisha beki wa kati wa Mbeya City, Juma Nyosso kufungiwa mechi zaidi ya Saba na kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
Gazeti kiongozi la michezo nchini, la Championi katika toleo la Ijumaa wiki iliyopita, limeibua mapya katika ulimwengu wa soka la Tanzania, baada ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kumpiga kitanzi cha mechi nane (8) beki tegemeo wa Mbeya City, Juma Nyosso kwa kitendo cha udhalilishaji alichokifanya kwa straika wa Simba, Elias Maguri katika mchezo kati ya timu hizo Jumatano, wiki iliyopita.
Uhuni wa hali ya juu huu
Pia kupitia vyombo vya habari, TFF imemtia hatiani beki wa Azam, Agrrey Morris kwa kosa la kumpiga kiwiko straika wa Simba, Emmanuel Okwi, huku pia rungu hilo likimsubiri beki wa Ruvu Shooting, George Michael Osei kwa kitendo cha kumkaba 'kinyama' straika, Amissi Tambwe.
SOMA KWA UDANI....
KAMATI YA NIDHAMU YAWAADHIBU NYOSO, MORRIS
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City
na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya wakiwa
uwanjani.
Gazeti la Championi Ijumaa, lililochapisha 'upuuzi' uliofanywa na Nyosso katika mchezo huo, ambapo inatafsiriwa gazeti hili ndilo lilikuwa chanzo cha yote. |
Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya
udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara
ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu)
jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba
radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili
Jerome Msemwa alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa,
kudhalilisha utu wa mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira
wa miguu.
Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa
hatiani kwa kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana
kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa
Morris alikiri kugongana na Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye 'reli' ndiyo
ukatokea mgongano huo.
Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti
za Brain CT scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya
Mifupa Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa
kichwani akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video
uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.
Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya
48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo
tatu na kumpa onyo kali.
Pia Kamati hiyo imemfungia miezi sita na kumpiga faini ya
sh. 200,000 Meneja Vifaa (Kit Manager) wa timu ya Polisi Mara, Clement Kajeri
kwa kuhamamisha vurugu na kuwapiga waamuzi kwenye mechi dhidi ya Mwadui
iliyochezwa Uwanja wa Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia
kanuni ya 40(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Wachezaji watatu wa Friends Rangers; Mahmoud Othman, Khalid
Twahil na John Alexander wamefungia miezi sita na faini ya sh.
Licha ya wachezaji hao kuitikia mwito wa Kamati, wachezaji
hao walizuiwa na viongozi wa kuingia ukumbini wakati malalamiko dhidi yao
yalipoanza kusikilizwa. Hatua hiyo iliifanya Kamati ifanye uamuzi baada ya
kuusikiliza upande wa walalamikaji pekee.
MBAYA WA TAMBWE ATOKOMEA...
Shauri dhidi ya mchezaji George Michael wa Ruvu Shooting kwa
kumchezea ubabe Amisi Tambwe wa Yanga, Kamati imeliahirisha baada ya
mlalamikiwa kupata udhuru uliosababisha asiwepo. (Michael alionekana kumkamia Tambwe katika mchezo baina ya timu hizo mbili ambapo Tambwe alitoka uwanjani akivuja damu huku pia picha zilizochapishwa na Championi Jumatatu wiki iliyopita, lilikuwa chombo pekee kilichochapisha 'uozo' huo).
Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu ya
Friends Rangers kupinga refa kuchezesha mechi yao dhidi ya Majimaji kwenye mvua
kubwa, kutoa maamuzi yasiyo halali na kutokuwepo na ukweli kwenye ripoti ya
Kamishna yakasikilizwe na Bodi ya Ligi kwa vile si masuala ya kinidhamu.
No comments:
Post a Comment