Hakuna jingine zaidi ya dua za Watanzania kwa ujumla, awe mtu wa Simba au wa Majimaji, kila mmoja anahitajika kuomba kwa moyo mkunjufu, kuiombea Yanga ambayo leo ndio siku pekee ya kujua hatma yake kwenye michuano ya kimataifa, watakaposhuka dimbani kumenyana na wanajeshi wa Botswana, BDF XI.
Mechi hiyo itapigwa leo majira ya saa mbili usiku huko Labtse, mji ulio takribani KM 70 kutoka mji mkuu wa Botswana, Gabrone.
Nahodha na beki tegemeo wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ pamoja na straika Kpah Sherman wamefunguka na kuwaomba Watanzania bila kujali uhamisimu, kuiombea kwani inawalikilisha taifa na haiku kule kama Yanga klabu.
Wakizungumza na blogu hii kwa njia ya mtandao kutoka Botswana, Cannavaro alisema, “Muhimu sala, Watanzania watuombee na sisi hatutawangusha. Cha msingi ni kucheza kwa nidhamu, naamini tutaweza kufanikiwa.
“Uzuri hali ya hewa ya hapa (Botswana), haitofautiani na nyumbani, ila hapa ni baridi kidogo lakini sio kesi kusema kuwa inaweza kutuathiri na tusishwe kucheza. Mungu kwanza jamani,” alisema Cannavaro huku Sherman naye akiongez; “Inshallah tutafuzu, japo mchezo hautakuwa mwepesi.”
Katika mchezo wa leo, Yanga inahitaji sare yoyote ilea ma hat aikifungwa isiruhusu mabao 2-0, kutokana na kujiwekea kibindoni hazina ya mabao 2-0 katika mchezo wa awali uliopigwa wiki mbili zilizopita hapa Bongo. Mabao yote yakifungwa na Amissi Tambwe.
No comments:
Post a Comment