Monday, February 16, 2015

ANGALIA VIWANGO VYA WACHEZAJI WA YANGA vs BDF XI



Tambwe kushoto na Msuva na Ngassa wakishangilia moja ya bao kwenye mchezo na BDF.

Wikiendi hii, Yanga ilifanya kweli mbele ya wanajeshi wa Botswana, BDF XI kwa kuwachapa mabao 2-0, ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho, hatua ya awali.

Amissi Tambwe atabaki kuwa staa wa mchezo huo, kwa kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao yote na kuipa matumaini kiasi kadhaa ya kusonga mbele, japo bado roho ya Yanga iko mikononi mwa Waswana hao kutokana na aina ya mchezo wa waliocheza juzi.

Achana na kichapo, Waswana walionekana kuwa watu hatari na waliingia na akili ya kucheza soka la kujilinda zaidi badala ya kushambuliaji, kwa mantiki kwamba wataisubiria Yanga. Ni dhahiri jamaa wako vizuri na hiyo ilithibitishwa na mashambulizi machache waliyofanya langoni kwa Yanga lakini yenye hatari kubwa.

Pluijm.
Hata kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm alikiri kwamba bado wana kibarua kigumu na alitambua mapema kwamba walitua nchini kusaka walau pointi moja kwa soka la kujilinda, hivyo kuwapa uhuru Yanga kujimwaya kwenye mchezo wa juzi Jumamosi. Zifuatazo ni alama za wachezaji wa Yanga katika mchezo huo. BOFYA read more kuangalia viwango

Kipa, Ally Mustafa ‘Bartez’ 6.5


Licha ya kwamba ana ‘clean sheet’ nzuri kwa sasa, ukiwemo mchezo wa juzi kutoruhusu bao pamoja na kuondoa hatari kadhaa langoni, lakini kwa asilimia kubwa ni kama alikuwa likizo. BDF walicheza soka la kujilinda zaidi na mashambulizi ya kushutukiza na aliweza kukaa vema kwa sapoti kubwa ya mabeki.
Lakini kosa la ‘kitoto’ la kuchelewesha muda na kupewa kadi ya njano, lilimshushia hadhi yake kwenye mchezo huo, kwa mantiki kwamba katika mchezo wa marudiano, anatakiwa kuwa makini zaidi, vinginvyo anaweza kuigharimu Yanga ikiwa itafuzu hatua hii, kwamba akipewa kadi tatu, basi lazima akae nje kutumikia adhabu ya kadi.
Beki kulia, Mbuyu Twite 7
 
Kiraka anayefahamika kwa uwezo wa kucheza kila idara, alikuwa mzuri katika kupandisha mashambulizi akisaidiana zaidi na wingi, Simon Msuva lakini alikuwa na makosa kadhaa ya kuruhusu mashambulizi.
Mfano kipindi cha kwanza, alifanya kosa kubwa la kumvuta jezi winga hatari Kabelo Seakanyeng kwenye hatari, japo mwamuzi Thiery Nkurunzinza kutoka Burundi hakuliona. Iwapo mwamuzi angeliona, maana yake ni kwamba Yanga ingejipa mzigo mwingine.
Beki kushoto, Oscar Joshua 6.3

Hakufanya kosa la msigi kama beki, lakini alikuwa na madhaifu makubwa katika kuiunganisha timu, asilimia kubw aya pasi zake zilinaswa na wapinzani, hususan zile alizopiga katikati, jambo ambalo liliwapa kazi ya ziada viungo kuusaka mpira tena. Pia kama beki wa pembeni, hakufanya mashambulizi ya kweli kwa kupiga krosi za kuwalisha mastraika.
Beki nne, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ 8


Pacha yake ya Kelvin Yonda ‘Cotton’ ilikuwa ya kipekee siku hivyo na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kumkamata vilivyo fowadi wao, Vicent Nzombe. Alikuwa naye bega kwa bega kuhakikisha haleti madhara langoni mwa Yanga.

Kilichompa heshima zaidi katika mchezo huo, ni hatari baada ya Master Masitara kuwazidi ujanja mabeki na viungo na kutoka nayo kwenda langoni, lakini kwa ushujaa zaidi, Cannavaro aliteleza na kutoa mpira huo, jamaa akiwa uso kwa uso na Bartez.
Beki tano, Kelvin Yondan 7.5 
Yondan kushoto akimkabili fowadi wa BDF.
Kama ilivyokuwa kwa Cannavaro, Yondan hakuw ana papara na alifanikiwa ku-control mipira yote ya juu na alikuwa na mawasiliano mazuri na pacha wake, Cannavaro siku hiyo. Dosari ndogo ambayo ni lazima ‘idara’ ya ulinzi kulifanyia kazi, suala la kujisahau kwa kupanda wote na kumuacha kipa asiwe na ulinzi wa kutosha.
Na hiyo ilionekana kuwasumbua sana Yanga katika mchezo huo, kwani kwa timu yenye wachezaji wenye mbio, mfano kama Ngassa, Msuva ama Mbeya City inaweza kuwagharimu sana Yanga. Kwa nafasi ya Cotton ndiye mwenye jukumu la kumlinda kipa na sio beki nzima kupanda bila kubaki mtu wa kumlipa Bartez.
Kiungo mkabaji, Salum Telela 6
Telela kushoto.
Yanga haikuwa na nguvu katika nafasi hii, pamoja na kwamba bado ‘anagain’ lakini Telela hakuwa kwenye ubora wake, na kwa mchezo wa wapinzani wao-kupaki basi, ilikuwa fursa pekee kwa Telela kupika pasi cha uchochezi kwa msaidizi wake (no.8), lakini muda mwingi alikuwa akipiga pasi za nyuma (back passes) kutaka kuwavuta wapinzani.
Ukichahilia pasi zake nyingi kunaswa, lakini pia alipitwa mara kadhaa na wageni walionekana kuwa wajanja, wenye kasi kuliko yeye, jambo ambalo liliwapa kazi ya ziada walinzi kuzima mashambulizi yaliyotokana na ‘maboko’ ya Telela.
Winga kulia, Simon Msuva 6.5
Msuva kushoto.
Hakuwa Msuva aliyezoeleka kwa kasi, krosi na makeke kwwa wapinzani, licha ya kucheza dakika zote, pamoja na kuchangia katika bao la kwanza, lakini hakuwa kwenye ubora wake. Alikuwa na krosi chache, licha ya kubadilishana nafasi ya Andery Coutinho pamoja na Mrisho Ngassa, lakini hakuwa na madhara kiviiile na alionekana kabisa kushindwa kumzidi ujanja beki, Othusitse Mpharitlhe.
Kiungo mshambuliaji, Haruna Niyonzima 7.8
Niyonzima katikati.
Alikuwa mtu hatari kwa Waswana siku hiyo hususan kipindi cha kwanza, alichangia bao la kwanza, kwa krosi yake murua na kumkuta Tambwe aliyemalizia. Pasi zake za kila aina-ndefu kwa fupi, majonjo ya kuvutia pamoja na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuteka safu ya kiungo cha kati cha wapinzani.
Hata hivyo kidogo kipindi cha pili dakika za 70 kuelekea 80, alionekana kuchoka na pasi nyingi zilianza kunaswa, hivyo kuwaachia nafasi wapinzani kuwashambulia kama nyuki.
Senta fowadi, Amisi Tambwe 8
Tambwe aliyekumbatiana na kocha Pluijm akishangilia bao lake la kwanza.
Licha ya kwamba hakuwa katika kiwango kizuri sana kama fowadi, lakini mabao muhimu sana ka timu yake yanabaki kuwa kielelezo cha heshima yake kwenye mchezo huo.
Alitumia vema krosi mbili zilizochongwa na Niyonzima na Mrisho Ngassa na kuisaidia Yanga kujiweka katika nafasi nzuri katika mchezo wa marudiano. Lakini ki uhalisia, hakuwa mzuri ki uchezaji, labda atumie kigezo cha mshambuliaji wa mwisho (yaani mtu wa kusubiri mipira na kuweka kambani).
Hakuwa na nguvu mbele ya Mompati Thuma na Keleagetse Mogomotsi na kwa asilimia kubwa walikuwa ‘free’ sana kutokana na ‘unyonge wa Tambwe. Ndiyo maana kocha Pluijm alimpumzisha na nafasi yake kuchukuliwa na Jerry Tegete.

Staika wa pili, Mrisho Ngassa 7.9
Ngassa kushoto akijaribu  kumtoka beki Mpharitlhe wa DBF XI
Anafahamika kama winga hatari, lakini siku hiyo alicheza sambamba na Tambwe katikati, alikuwa mtu hatari sana kwenye safu ya mabeki na alikuwa mjanja sana kuwatoroka akisaidiwa zaidi na kasi yake. Kocha wa DBF Letang anaamini ndiye mtu aliyewaua siku hiyo kutokana na ‘flexibility’ yake uwanjani kwa kubadilisha nafasi.
Ndiye mpikaji wa bao la pili, baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa DBF na kuachia krosi murua iliyomkutan Tambwe na kukwamisha mpira dakika ya 55. Kosa lake moja tu, ni kushindwa kucheza nafasi yake, kwani asilimia kubwa alijikita akicheza kama winga licha ya mwalimu kumpanga kati.

Winga kushoto, Andrey Coutinho 7
Makeke yalipungua kwa kiasi fulani, aliachia krosi mbili hatari japo zilinaswa na Waswana. Alikuwa mzurzi katika kupandisha mashambulizi na kufanya kazi ile ya maana ya kuitwa winga, lakini kipindi cha pili aliishiwa pumzi hivyo Pluijm kumpumzisha dakika ya 71 na nafasi yake kuchukuliwa na Kpah Sherman.

Sub
Jerry Tegete 5


Kpah Sherman 5

Sherman mwenye mpira.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...