Pogba awekwa sokoni rasmi! dau lake euro Mil.100 |
Licha ya kusaini mkataba mpya, kiungo wa Juventus, Paul Pogba imefahamika kuwa anaweza kuondoka klabuni hapo baada ya msimu ujao.
Wakala wa nyota huyo raia wa Ufaransa, amesema anaamini ataondoka Juve mapema baada ya kumalizika kwa msimu ujao.
Hivi karibuni, Pogba aliongeza mkataba utakaomfanya kubaki Turin hadi 2019, lakini ni lulu
Ulaya kwa sasa huku klabu lukuki zikimuwania.
Wakala wake, Mino Raiola amesema, "Mkataba mpya aliouongeza yalikuwa ni maamuzi ya haraka na rahisi. Sio kusema kusaini mkataba mpya kumeleta matatizo Juventus, hapana."Nataka timu zinazomuhitaji, naamini zitakuwa tayari kumnunua.
Iwapo Paul ataondoka Juve, hakika ni haki yake, kama hilo halitatokea msimu huu, basi mwakani," alisema wakala wake na kuendelea;"Paul yupo katika kiwango mastaa wengine kiuchumi
na anaheshima sawa na hao.
na anaheshima sawa na hao.
"Lakini tofauti na hao mastaa wengine, Paul ni staa anayepatikana baada ya msimu huu.
Kama huwezi kuwanunua Cristiano Ronaldo, Lionel Messi au Zlatan Ibrahimovic, basi unaweza kumchukua Paul.
"Thamani ya nyota huyo wa zamani wa Manchester United inadriwa si chini ya euro milioni 100, kwa mujibu wa wakala wake.
No comments:
Post a Comment