Anatakiwa Emirates... Kiungo chipukizi wa Valencia, Jose Gaya anahitajika na klabua ya Arsenal kwa vyovyote vile!
|
Klabu ya Arsenal imeanza
mazungumzo na Klabu ya Valencia ya huko Hispania, kutaka saini ya kinda wao Jose Luis
Gaya, baada ya kumtengea kitita cha pauni milioni 13.5.
Kwa mujibu wa Gazeti la The
Express tayari Arsenal wameweka hadharani nia
hiyo.
Hata hivyo kinda huyo amekuwa
akitolewa macho na vigogo wa hela
duaniani, Real Madrid lakini bado haijajulikana kama Arsenal wataendelea moto
huo baada ya Madrid kuingilia dili lao mchana leo hii.
Klabu yake ya Valencia haina matarajio ya kumuachia kinda huyo lakini 'mzigo' wa maana ambao
wanaweza kutengewa na klabu nyingine hususan za England, zitawashawishi kumuachia kinda
huyo.
No comments:
Post a Comment