Hatimaye kikosi cha Manchester City kilicho chini ya kocha mkuu ‘Manuel Pellegrini’ kimeweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England maarufu kama EPL baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2 – 0 dhidi ya wagonga nyundo wa jiji la London Westham United katika mtanange wa mwisho wa kufunga pazia la ligi kuu hiyo inayoongoza kwa kutazamwa na wapenzi wengi wa soka Duniani.
Wachezaji wa Manchester City wakiwa wamemnyanyua juu kocha wao Manuel Pellegrini ikiwa ni ishara ya kuonyesha ni jinsi gani walivyokuwa na furaha
Mabao ya City yalifungwa na Samir Nasir baada ya kupewa pasi nzuri kutoka kwa kiungo mshambuliaji Yaya Toure huku goli la pili likifungwa na Vicent Kompany. Mchezo mwingine uliokuwa wa vuta nikuvute ni ule ulioikutanisha klabu ya Liverpool waliowakaribisha nyumbani NewCastle United ambao walikubali kipigo cha bao 2 -1 kutoka kwa majogoo hao wa London katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la Anifield jijini humo.
Magoli ya Liverpool yalifungwa kupitia mshambuliaji wake hatari Daniel Sturridge pamoja na Daniel Agger aliyesawazisha huku bao pekee la kufutia machozi kwa Newcastle likipatikana baada ya mchezaji wa Liverpool Martin Skrtel kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira.
Wachezaji wa Liverpool wakiwa wamekosa furaha licha ya ushindi wa bao 2 -1 dhidi ya NewCastle lakini haikuwa muarobani kwa Man City walioibuka mabingwa
Matokeo hayo yameiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa huo mkubwa kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu wa mwaka 2011/12 pamoja na 2013/14 huku ikimaliza kileleni mwa ligi hiyo kwa jumla ya pointi 86, wakati wapinzani wao wanaowafuatia ‘Liverpool’ wakiwa nyuma yao kwa tofauti ya pointi mbil tu huku Norwich City, Fulham pamoja na Cardiff zikijikuta zikishuka daraja.
Mashabiki wa Liverpool wakiishangilia timu yao
Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na Cardiff iliyokubali kipigo cha bao 1 -2 toka kwa Chelsea, Fulham ikitoka sare ya 2 – 2 na Crystal Palace wakati Norwich ikiloweshwa goli 0 – 2 kutoka kwa washika mtutu wa jiji la London ‘Arsenal, Southampton ikiilzamishana sare ya bao 1 – 1 na Manchester United, Sunderland wakichezea bao 1 – 3 toka kwa Swaswea City, Tottenham Hotspurs ikiigalagaza 3 -1 Aston Villa na mwisho kabisa ni West bromwich Albion iliyopokea kipigo cha 1 – 2 toka kwa Stoke City.
No comments:
Post a Comment