Monday, May 12, 2014

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA NZEGA KWA KUKAGUA MIRADI MUHIMU YA HUDUMA ZA JAMII NA MIKUTANO MIKUBWA YA HADHARA.LEO KUANZA ZIARA WILAYA YA UYUI




Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishuka kutoka juu ya tanki, wakati akikagua mradi wa maji wa Itobo, wilayani Nzega, jana Mei 11, 2014, alipokuwa akiendelea na ziara yake ya siku kumi katika mkoa wa Tabora, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa juu ya tanki hilo la mradi wa maji wa Itobo, wilayani Nzega, jana Mei 11, 2014, akiambatana na Kinana katika ziara ya siku kumi katika mkoa wa Tabora, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi katika Halmashauri ya Nzega, Samweli Buyigi (kushoto), kuhusu bwawa la chanzo cha maji kilichopo katika halmashauri hiyo ambalo limekauka kutokana na kuota magugu maji. Watatu kushoto ni Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala.

Kinana akikagua chujio la maji la Mamlaka ya Majisafi Nzega mkoani Tabora, Pamoja naye ni Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangala, na anayempa maelezo ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi Nzega, Samweli Buyigi Mkurugenzi (kushoto)

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akijadili jambo na Kigwangala wakati akikagua miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi mji wa Nzega, jana Mei 11, 2014.

Mbunge wa Viti Maalum Munde Tambwe (kushoto) akimsaidia kutia mchanga kwenye mashine ya kufyatulia mafotali, Katibu Mkuu wa CCM, Kinana aliyekuwa akishiriki kufyatua matofali ya mradi wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Nzega, jana Mei 11, 2014. Kushoto ni Kigwangala

Mjunbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Hussein Bashe, akitaja mchango wake wa fedha taslim sh. 500,000 na ahadi ya kiasi hicho hicho cha fedha kuchangia mradi wa ufyatuaji matofali wa kina mama wa UWT wilaya ya Nzega mkoani Tabora ambao umezinduliwa na Kinana (kulia), jana Mei 11. 2014. Wapili kulia ni Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangala na Mbunge wa Bukene wilayani Nzega, Suleiman Zedi ambaye pia alichangia mradi huo sh. 500,000.

Katibu Mkuu wa CCM Kinana na wakati Mbunge wa Nzega, Kigwangala wakitangaza kutoa mchango wa sh. 500,000, wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa ufyatuaji matofali wa UWT Nzega

Bashe na Kigwangala wakimwaga kicheko wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa ufyatuaji matofali wa kina mama wa UWT

Jengo la kisasa la soko jipya la Kata ya Itobo, Nzega ambalo limejengwa na serikali hili karibuni na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kulikagua jana Mei 11, 2014

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya jana Mei 11, 2014 katika kijiji cha Itobo wilayani Nzega

Wananchi wa Itobo wakimsikiliza kwa makini Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho jana Mei 11, 2014

Katibu Mkuu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape akihutubia kwenye mkutano huo wa Itobo

Wanachama wa zamani na wapya wa CCM wakilakiapo cha utii wa CCM wakati wanachama wapya zaidi ya 85 walipokabidhiwa kadi za CCM

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akitazama bwawa ambalo hutumiwa na mwananchi wa kijiji cha Bukene, katika kilimo cha mpunga cha umwagiliaji
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika Uwanja wa Taifa wa Bukene, wilayani Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara jana Mei 11, 2014, mwishoni mwa ziara yake wilayani Nzega kabla ya kuanza kesho ziara katika wilaya ya Uyui. Picha zote na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...