Monday, January 20, 2014

TIGO YAJA NA PROMOSHENI YA RUDISHIWA PESA YAKO


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

‘Rudishiwa Pesa yako’

Tigo kuwarudishia wateja wake gharama za kununulia laini za simu
Dar es salaam, Januari 202014 – Katika jitihada za kuwapa watanzania wengi fursa yakupata huduma za mawasiliano ya simu, Tigo leo imezindua utaratibu wa kuwarudishia wateja wake gharama zote manunuzi ya laini za simu kwa kuwapa muda wa maongezi na kuwapa salio katika akaunti zao za Tigo Pesa.

Akizindua kampeni hiyo iitwayo “Rudishiwa Pesa Yako” katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, amesema kuanzia sasa wateja watakaonunua laini mpya za Tigo kwa gharama 1000/- watapewa muda wa maongezi wa 500/- na kuwekewa salio la 500/- nyingine katika akaunti zao za Tigo Pesa.

“Hii inamaanisha kwamba mteja atakuwa anapata laini mpya ya Tigo bure kwa kurudishiwa gharama zote za manunuzi na hii ndio maana ya kuiita kampeniyetu ‘Rudishiwa Pesa Yako’”amesema.
Mpinga amesema kampeni ya ‘Rudishiwa Pesa Yako’ inalenga katika kuwapa fursa watanzania wengi zaidi uwezo wa kupata huduma za mawasiliano yaliyo bora na ambayo yanaweza kuwa chachu katika kualetea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

“Tigo inazidi kuwapa fursa watanzania zaidi na zaidi za kuwasiliana na jamaa na marafiki zao.Hii ni fursa mojawapo kwao kukuza biashara zao, kutuma na kupokea pesa kupitia akaunti zao za Tigo Pesa na huduma nyingine nyingi ambazo tunatoa,” alisema.

Katika kuhakikisha ubora wa huduma kwa wateja wake wapya na wa zamani, Mpinga amesemamwaka jana Tigo iliendelea kufungua maduka zaidi ya kuwahudumia wateja na kujenga zaidi ya minara 500 mipya “ili kuboresha mawasiliano na kuwafikia wateja walioko maeneo ya vijijini yasiokuwa na mawasiliano ya simu.”

Mpingaamesemakampuni hiyo itatangaza kampeni ya Rudishiwa Pesa Yako kupitia njia mbalimbali zikiwemo redio, TV na mabango “kwa lengo la kuwafikishia ujumbe watanzania wengi iwezekanavyo kuhusu ofa hii kabambe.”

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...