Thursday, January 23, 2014

MCHEZAJI WA CHELSEA JUAN MATA ATUA MANCHESTER UNITED RASMI



Juan Mata.

MANCHESTER United imekubali kulipa ada ya pauni milioni 37 ambayo ni rekodi kwa klabu ili kumnasa Juan Mata kutoka Chelsea na hii inasaidia kidogo kupoza machungu ya kutolewa Capital One Cup. Bosi wa Chelsea Jose Mourinho ameidhinisha dili hilo baada ya mazungumzo na maofisa wa klabu na sasa Mata anategemewa kufanya vipimo vya afya jijini Manchester kesho Alhamisi.

Mtendaji mkuu wa Manchester United amekubali kuvunja rekodi ya klabu ya usajili kwaajili ya Mata ili kuokoa msimu unaokwenda kombo kwao.

Vipigo saba katika Ligi Kuu ya England vimeiacha United ikiwa nyuma kwa pointi 6 kutoka nafasi ya nne kwanye msimamo wa Ligi ambayo ingewawezesha kushiriki Champions League msimu ujao – lakini kuongezeka kwa Mata kunatarajiwa kuleta uhai mkubwa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...