Friday, January 17, 2014

HUU HAPA MZIGO MPYA WA JACK WOLPERStaa wa Filamu Bongo Jacqueline Wolper akiwa kwenye pozi na mchumba wake mpya

Jacqueline Wolper akiwa na mchumba wake wa sasa G. Modo.
Stori: IMELDA MTEMA
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Wolper alisema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya kutafakari kwanza maana asingeweza kukurupuka wakati bado hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake huyo. “Kiukweli nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja kwa moja kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na Mungu, ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi niliyempata ni sahihi kwangu,” alisema Wolper.
Wolper aliongeza kuwa kama siku Mungu atajalia kwa mpenzi wake huyu kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja kwa wazazi wa pande zote mbili ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho anakiomba kila kukicha.
Jack Wolper akiwa kwenye pozi tofauti tofauto

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...