Friday, September 27, 2013

TIMU YA CHELSEA FC YATWAA KOMBE LA SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA MWANZA

Meneja Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga (kushoto),akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Chelsea ya Mabatini Mwanza jioni ya leo baada ya kuibuka kidedea kupitia matuta.
TIMU ya mpira wa miguu ya Chelsea FC ya Mabatini Mwanza, leo imefanikiwa kutwaa Kombe la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililokuwa likifanyika jioni ya leo katika uwanja wa Polisi Mabatini,ambapo timu zaidi ya nane zilichuana na hatimaye kumpata mshindi,aliyejinyakulia kikombe na kitita cha shilingi laki 3 kwa mshindi wa kwanza huku mshindi wa pili akipewa kitita cha shilingi laki 2.

Nahodha wa timu hiyo akiwa amenyanyua kombe juu na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo.

Baadhi ya mashabiki wa timu ya Chelsea wakishangilia baada ya kushinda kwa njia ya matuta.

Mwakilishi wa Bia ya Serengeti wa Mwanza Mwanza Joan Semuguruka (kushoto), akimkabidhi kitita cha shilingi laki mbili  Nahodha wa timu ya FC Barcelona  kama zawadi ya  mshindi wa pili kwenye mpambano huo.

Joan Semuguruka(kushoto),akimkabidhi kitita cha shilingi laki 3 Nahodha wa timu ya Chelsea,huku akishuhudiwa na Meneja wa Vipindi vya Clouds FM, Sebastian Maganga aliyesimama katikati yao.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo wakishuhudia mpambano huo.

Timu ya Arsenal, ikipambana na Timu ya FC Barcelona ya Mabatini katika moja ya mchezo wa Nusu fainali,ambapo Barcelona iliibuka na ushindi na kutinga hatua ya Fainali.

Mmoja wa wachezaji wa timu ya Real Madrid ya Kirumba, akipiga penalty kwenye mpambano wa kuwania kufuzu hatua ya kuingia fainali ya mchezo huo, ambapo Real Madrid ilifukwa kwa mkwaju na timu ya Chelsea.

Mtangazaji wa Clouds FM, Anord Kayanda aliyesimama katikati ya mashabiki,akitangaza matokeo ya mechi hizo kabla ya kufikiwa kwa hatua ya fainali.

Meneja wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga,akiwamiminia Bia ya Serengeti baadhi ya mashabiki walifika kushuhudia baadhi ya mechi zilizokuwa zikiendelea Kiwanjani hapo.
Kati ya mashabiki waliohudhuria Kiwanjani hapo wakifatilia baadhi ya matukio yaliyokuwa yakijili uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...