Monday, September 23, 2013

SHAMBULIO LA KIGAIDI NAIROBI HALI YAZIDI KUWA MBAYA


-Milio ya risasi yasikika kutoka ndani ya jengo
-Moshi mkubwa unatoka kwa sasa
-Waliouawa wafikia 69, majeruhi 175
-Magaidi wawili wameripotiwa kuuawa leo asubuhi
-Yadaiwa magaidi wote ni wanaume
HALI ya sintofahamu imeendelea eneo la jengo la Westgate lililopo jijini Nairobi lililovamiwa na magaidi wa Al Shabaab tangu Jumamosi mchana.
Milio ya risasi imesikika kutoka ndani ya jengo ikifuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo lenye maduka na migahawa zaidi ya 80. Mpaka sasa hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo mkubwa na idadi ya mateka. Taarifa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, ni kwamba magaidi wawili wameuawa leo asubuhi na waliovamia jengo hilo wote ni wanaume.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...