Wednesday, September 4, 2013

KAMPENI YA TUKO WANGAPI,TULIZANA YAJA UPYA


Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt Donald Mmbando akizindua awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam.

SERIKALI imekiri kwamba mahusiano ya kingono na wapenzi zaidi ya mmoja ni changamoto kubwa hapa nchini na ni tabia ambayo inaleta athari kubwa kiafya na kijami.

Akizungumza na wanahabari leo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt Donald Mmbando amesema utafiti umeonyesha kwamba, mahusiano ya kingono na wapenzi wengi ni miongoni mwa vichocheo vinavyosababisha kuenea kwa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa haraka na kwa kasi kubwa.

Amebainisha kuwa tabia hatarishi ya kuwa na mahusiano ya kingono na wapenzi wengi imejikita katika jamii yetu hususani mahali pa kazi, shuleni na vyuoni.

Dkt Mmbando amesema hayo kwenye uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! ambapo alibainisha kuwa matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI na Malaria nchini kwa mwaka 2011/2012 yanaonyesha kwamba, maambukizi ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa wanawake na wanaume wenye mahusiano ya ngono na wapenzi wengi ni asilimia 7.5.

Nae Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi, Dkt Angela Ramadhan amesema tume hiyo itaendelea kutumia njia mbalimbali katika kuhamasisha mabadiliko ya tabia ya mahusiano ya kingono na wapenzi wengi.

Amesema awamu hiyo ya pili iliyozinduliwa jana inajikita katika kuhamasisha watu kujitoa katika mtandao wa ngono na kutulizana na vilevile kuimarisha mahusiano kati ya wenza.

Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi, Dkt Angela Ramadhan akimpa mkono DK. Donardi Mmbando mara baada ya kumaliza kutoa hotuba fupi ya Uzinduzi wa kampeni mpya ya Tuko wangapi Tulizana ,inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).
Kaimu Mkurugenzi wa USAID, Andrew Rebold, akitoa neno la utangulizi kabla ya mgeni rasmi kukaribishwa kwaajiri ya uzinduzi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa USAID, Andrew Rebold (kulia), akiongea jambo na Prezidaa wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat, muda mfupi kabla ya uzinduzi huo.
Moja ya wadau waliokuwa wamehudhuria kwenye uzinduzi huo wakiongea jambo.

Mwanamuziki wa Bendi ya Fm Academia, ambaye ni rais wa Vijana, Nyoshi El Saadat akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana!

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...