Thursday, September 19, 2013

AIRTEL,TRA ZAWAWEZESHA WATEJA WAKE KULIPIA LESENI ZA MAGARI‏

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla (wa pili kushoto) akifuatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel Money wakishuhudia kulia ni Meneja kitengo cha Airtel Money John Ndunguru, mwisho kushoto ni mwakilishi wa Max Malipo Tumsifu Lema.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money pichani kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba. Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs.Diana Masalla (wa pili kushoto) akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel Money.

Press Release
Airtel yashirikiana na TRA kuwawezesha wateja kulipia ada za lesseni za magari Airtel Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania TRA wamezindua rasmi huduma ya kufanya malipo ya ada za leseni za magari kupitia huduma ya Airtel money. Huduma hii inapatikana bure kwa wateja wote wa Airtel nchi nzima. Hii inawawezesha watumiaji wa huduma hii kulipia leseni ya magari yao wakiwa ofisini au majumbani mwao kwa urahisi zaidi ambapo kwa sasa ni BURE.

Adriana Lyamba, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel amesema " huduma ya kulipia leseni ya magari kupitia Airtel money imeleta unafuu kwa wateja watakaotaka kulipia leseni za magari. Huu ni mwendelezo wa mapinduzi ya huduma za kifedha kupitia huduma ya Airtel money inayomuhakikishia mteja uharaka, unafuu, usalama na urahisi zaidi katika kulipia huduma mbalimbali. Tunaamini huduma hii ya kulipia leseni za magari kupitia Airtel money kutaleta ufanisi na kuendeleza juhudi za serikali katika ukusanyaji wa kodi. Tunaahidi kuendelea kuleta suluhisho katika huduma za malipo mbalimbali na kuwahakikishia wateja wetu urahisi, usalama na ufanisi zaidi kupitia Airtel Money."

Sasa tumewawezesha wateja wote wa Airtel kulipia leseni za magari bila kuwa na haja ya kutembelea ofisi za TRA kufanya malipo. Wateja watatakiwa kwenda kuchukua leseni/stika zao pale malipo yatakapofanyika na leseni/stika zao kuwa tayari Akiongea kuhusu huduma ya malipo ya ada za leseni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla alisema"
huduma hii mpya inahusisha malipo ya ada za lesseni za magari, ada za uamisho wa magari pamoja na malipo mengine ya ada za usajili wa magari. Huduma hii itawezesha ukusanyaji wa malipo ya ada / kodi zifanyike kwa njia rahisi na nafuu. Unaweza kupata kiasi cha kulipia ada unayotakiwa kulipia kisha ukalipia hapohapo ndani ya sekunde chache kupitia huduma ya Airtel money.

Ulipaji huu unaenda sambamba na kauli mbiu ya TRA ya Urahisi, Uhiari na Uboreshaji Endelevu Akiongea juu ya namna ya ulipiaji ada Meneja wa kitengo cha Airtel money John Ndunguru alisema" huduma hii inapatikana kwa wateja wa malipo ya awali na ya mwenzi

Aliongeza kwa kusema ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hii, Airtel imeweza kuiweka kwenye MENU ya Airtel Money "TRAMAGARI" ili kuweza kurahisisha ulipaji wa ada na kuiwezesa serikali kukusanya ada kwa gharama nafuu zaidi"

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga alisema "Ninawapongeza sana kampuni ya Airtel Kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kurahisisha ukusanyaji wa kodi hii ya Ada za magari maarufu kama Road License. Hi ni huduma nzuri inayosaidia watanzania kuokoa muda wao pale wanapoweza kutumia simu zao kupitia mtandao wa Airtel kulipia Ada ya magari yao kila mwaka bila usumbufu." Kwa urahisi huu inatusaidia sana kuokoa muda ambao ungepotea kukaa kwenye foleni ya malipo na badala yake muda tunaookoa tutautumia katika shughuli nyingine za kiuchumi.

Naomba niwakumbushe kuwa wiki ya usalama barabarani itaanza wiki ijayo tarehe 23.9.2013 hivyo mambo yote ya ukaguzi wa stika za ada za magari yaani (Road Licence) pamoja na Stika za usalama barabarani na ukaguzi wa vyombo vyote vya moto utaenda sambamba, hivyo ninawakumbusha watumiaji wote wa vyombo vyote vya moto kufuata sheria zote zilizowekwa ili kuepuka adhabu ya kulipa faini. Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja kutumia simu zao za mkononi katika huduma za kifedha zikiwemo kulipa bill ya maji DAWASCO, kulipia Luku TANESCO malipo ya DSTV, kulipia visa ya USA na sasa ada za lesseni ya magari. Airtel money ni huduma rahisi na salama inayotoa huduma za mobile benki na za malipo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...