Wednesday, December 19, 2012

YANGA YAPOKEA SH. MILIONI 105 KUTOKA KWA PRIME TIME PROMOTION



Mkurugenzi wa Prime Time, Joseph Kusaga akikabidhi hundi ya sh milioni 105 kwa makamu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kwa ajili ya kutumika katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Januari 19, mwakani.
************************
Kampuni ya Prime Time Promotion imeikabidhi mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga hundi ya shs Milioni 105 kwa ajili ya kutumika katika mkutano wake mkuu wa mwaka wa wanachama uliopangwa kufanyika Januari 19, mwakani.
Fedha hizo zilikabidhiwa katika mkutano maalum uliowakutanisha viongozi wa Yanga na wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kuwa klabu yake imeingia makubaliano na Prime Time kwa kusimamia shughuli zake zote ikiwa pamoja na mkutano huo.
Sanga alisema kuwa mbali ya mkutano huo, Prime Time itakuwa na jukumu la kuandaa mechi mbali mbali za kimataifa kwa ajili ya kuhimarisha kikosi chao na baadhi ya malipo yatachukuliwa na kampuni hiyo.
Alisema kuwa hatua hiyi ni ya kuifanya klabu yao kuwa ya kisasa zaidi na kutambua kampuni zenye uwezo wa kufanya shughuli mbali mbali kama Prime Time Promotion kufanya kwa niaba yao.
“Kuna kampuni zenye uwezo au utaalam wa kufaya matukio mbali mbali kama Prime Time ambazo zinatakiwa kupewa nafasi hiyo, uongozi hauwezi kufanya shughuli zote, tunataka kuendesha klabu kisasa zaidi,” alisema Sanga.
Nae Mkurugezi wa Prime Time Joseph Kusaga alisema kuwa makubaliano hayo yatahusisha pia mechi ya kimataifa itakayofanyika Januari 12 na 13 na shughuli nyingine za klabu hiyo ili kuongeza kipato.
Kusaga alisema kuwa wamevutiwa na Yanga kutokana uongozi wao kuongoza kwa uwazi zaidi na kuvutiwa hatua yao ya hivi karibuni ya kuweka mapato na matumizi wazi kwa wanachama na wadau wa michezo kwa ujumla.

Alisema kuwa huu ni mwanzo tu kwani kwa mwaka 2013 wamejipanga kufanya kazi na vilabu vyote nchini ili kukuza na kuendeleza mchezo huo. Kituo cha Televisheni cha Clouds kinatarajia kuonyesha live mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...