Friday, December 14, 2012

KOFFI OLOMIDE AWASILI DAR KUWARUSHA MASHABIKI WA SEBENE JUMAMOSI LEADERS CLUB



Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi kutoka DRC-Kongo, Koffi Olomide, akipunga mkono kusalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana usiku wakati akiwasili pamoja na kundi lake zima la Quartier Latin,kwa ajili ya onesho lake litakalofanyika kesho siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba. Onesho hilo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker na kiingilio katika shoo hiyo kitakuwa ni sh. 10,000/= kwa mtu mmoja na kwa wale watakaokatia tiketi mlangoni watalipia sh. 15,000/= getini. Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga

Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide baada ya kuwasili jana usiku kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar. Koffee Olomide, alisema kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...