Sunday, December 30, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT.GHARIB BILAL AMJULIA HALI PADRI AMBROSE MKENDA

RAY AWAFUNGUKIA WABAYA WAKE.....






INAWEZEKANA ukawa unafanya kazi lakini baadhi ya watu wakawa wanaziponda kwa chuki zao, ambapo msanii anayefanya poa bongo kwenye tasnia ya filamu Vicent Kigosi ‘Ray’, amesema kuwa wapo baadhi ya wasanii wenye tabia hizo na kudai kama wanaziponda kazi zake basi ni wachawi na wanachuki zao.

Mwandishi wetu alitaka kujua tabia hizo kama zipo katika tasnia hiyo, ambapo msanii huyo aliamua kuweka wazi kuwa popote penye mafanikio lazima kuwe na watu nwenye chuki huku akidai kuwa kuna wasanii wanaozichukia kazi zake kwa sababu anafanya vizuri sokoni kuliko wao.

Alisema kuwa mara nyingi watu wenye tabia hizo ni wale wasiyofanikiwa na kazi yao kubwa ni kusambaza ubaya juu ya watu wengine huku muda wao mwingine wakiutumia vibaya badala ya kubuni kazi za kufanya.

“Kuna watu wabaya sana mimi najua kuna baadhi ya wasanii ambao nipo nao karibu wanazichukia kazi zangu hasa pale zinapoenda sokoni, sijali na ndiyo maana nazidi kubuni kazi nzuri kila kukicha,” alisema.

QUEEN DARLEEN ATOA YA MOYONI



STAA anayefanya poa na ngoma ‘Kokoro’, Queen Darleen, ameuambia mtandao huu kuwa anajisikia raha kuwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wanawake, huku akiamini kuwa tabia za baadhi ya wanawake ndizo zinazomfanya awe hivyo.

Msanii huyo ni mmoja ya wanawake wenye staili za kipekee kabisa kwenye game ingawa ndani ya mwaka huu amekuja kivingine kabisa baada ya kuwa kimya kwa muda na kuteka mashabiki kupitia kibao cha ‘Maneno Maneno’.

Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya kuzungumza na mwandishi wetu alietaka kujua ni kundi gani la watu ambao hupenda kuwa nao karibu sana na kubandilishana mawazo ndipo yenye maana, ndipo alipofunguka kuwa mara nyingi huwa karibu na wanaume na si wanawake.

Alisema kuwa karibu na wanaume haimanishi kwamba ni mabwana zake hapana bali anaona ni watu ambao anaendana nao ingawa tabia zake si za kiume kama baadhi ya watu wanavyopenda kudhani kutoka na staili zake au aina ya kazi anazofanya.

“Kuna watu wanajua mimi nina tabia za kiume hiyo inawezekana kwa sababu wao ndo wanaosema, napenda sana kuwa na watu ambao tutafanya mambo ya maendeleo na si kuzungumza mapenzi na upuuzi muda wote hiyo ndo sababu kubwa inayonifanya nijiweke sana kwa wanaume,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa anahisi akijiweka karibu sana na wanawake hakuna kitu kikubwa watakachokuwa wanazungumza zaidi ya majungu na mapenzi, ingawa hata wanaume baadhi yao wako hivyo ila si kama wanawake ambao hupoteza mda mwingi kujadili ujinga.

"SIPO TAYARI KUZALISHWA KWA SASA"...BABY MADAHA



STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amefunguka kuwa hayupo tayari kuzaa kwa sasa.

Akizungumza kwa kujiamini, Baby Madaha aliweka wazi kuwa yupo bize sana na kazi zake za muziki na filamu hivyo suala la kunyonyesha litampotezea muda wake.

“We ubebe mimba sasa hivi, uilee halafu uje kunyonyesha, haya madili ya mjini yote yatafanywa na nani?” alihoji Baby Madaha na kuongeza:

“Mikakati yangu kwa mwaka 2013 ni kuhakikisha nafanya mapinduzi makubwa katika muziki wa Bongo Fleva na filamu.”

Saturday, December 29, 2012

ZITTO KABWE: UTAJIRI WA GESI ASILIA, TUWASIKILIZE WATANZANIA WA MTWARA NA LINDI. TUSIPUUZE


Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.

Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.

Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.

Mtwara na Lindi wanataka nini?
Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.
Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya Tumbaku.


Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali huru ya Tanzania?

Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.

Mtwara na Lindi wanakosea wapi?
Madai yao halali na mimi binafsi na chama changu tunayaunga mkono. Lakini kuna mahala lazima waelimishwe.
Watu wa Mtwara pia wanapaswa kuelewa kuwa juhudi zao zisiwatenganishe na Watanzania wengine kwani bado utajiri wa Taifa unafadisha kikundi cha Watanzania wachache sana. Watu wa Mtwara wanahitaji kuungana na watu wa Mara, watu wa Mwanza, watu wa Shinyanga na watu wa Kagera kudai utajiri wa nchi utumike kwa maendeleo ya watu badala ya kunufaisha kundi dogo la watu. Watu wa Mtwara wanapaswa kuunganisha nguvu na Watanzania wengine kuzuia uporaji wa rasilimali ya nchi dhidi ya kizazi kijacho. Watu wa Mtwara wasijitenge wakawa peke yao na Gesi yao. Nguvu ya mnyonge ni umoja.


Serikali isiyosikia
Serikali ina hoja kuhusu kujenga Bomba la Gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa gharama nafuu. Umeme unaotumiwa na asilimia 14 tu ya Watanzania. Kwa kuwa hii asilimia 14 ndio wenye sauti basi watu wa Mtwara wataonekana hawana hoja kabisa. Lakini Serikali imejiuliza mara mbilimbili kuhusu mradi huu wa Bomba? Tunaambiwa na Wataalamu kwamba kuna uwezekano mkubwa mwakani gesi asilia ya kiasi cha futi za ujazo trillioni 20 itakuwa imegunduliwa katika Kitalu namba 7( block 7) ambacho kipo mkoani Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke. Iwapo gesi nyingi hivi itakuwa hapa Dar karibu kabisa na mitambo ya kuzalisha umeme, mradi huu wa Bomba unaojengwa kwa trillioni za shilingi utakuwa na maana tena? Huu mkopo utakuwa na tija?


Serikali imewaambia watu wa Mtwara gharama za kuleta bomba Dar dhidi ya gharama za kujenga mtambo wa kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha umeme kwenda maeneo mengine ya Tanzania? Serikali imeangalia faida ya kujenga gridi nyingine badala ya kuwa na gridi moja tu yenye kushikwa na bwawa la Mtera? Leo bwawa la Mtera lisipozalisha hata megawati moja hata Dar es Salaam izalishe megawati alfu kumi umeme hautakuwapo maana uti wa mgongo wa gridi ni Mtera! Kwa nini tusiwe na gridi nyingine yenye uti wa mgongo Lindi au Mtwara?

Tuwasikilize watu wa Mtwara
Watanzania sio mabwege tena. Kuwaita watu wa Mtwara ni wahaini, wapuuzi au watu hatari haisaidii kujenga Taifa moja lenye watu huru. Serikali na wadau wote wa sekta ya Gesi likiwemo Bunge washirikiane na watu wa Mtwara kuhusu miradi ya gesi asilia. Tuwe na Azimio la Mtwara, tamko la kuelekeza namna bora ya kutumia utajiri wetu wa Gesi bila kuathiri umoja wa Taifa letu.

Ujio wa Sera, Maono na Uongozi Mbadala
Sasa hivi wananchi wa Mtwara kama wananchi wa sehemu nyingine wanahitaji maono mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala na mwelekeo mbadala wa kitaifa ambao utaangalia mahitaji yao, utazingatia raslimali zilizopo na utaunganisha utendaji wa sekta mbalimbali katika kutengeneza mfumo wa kiutawala na kiuchumi ambao utaliinua taifa zima.

Ni kwa sababu hiyo naamini chama changu ni jibu sahihi kwa matamanio na kiu ya wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine nchini. Ikumbukwe kuwa katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2010 tulielewa haja ya kuangalia mikoa hii ya Kusini kwa namna ya pekee na kuipa mwelekeo wa kipekee katika sera. Bado tuna makusudio hayo tunapoelekea 2015 na tukishika Dola wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine zote zilizoachwa pembezoni mwa mafanikio wajue kuwa wamepata rafiki na mshirika wa karibu wa kushirikiana nao kuleta maendeleo.

Siyo katika suala la gesi tu bali katika nishati, maji, elimu, miundombinu, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii. Mtwara kama ilivyo mikoa mingine ina raslimali za kutosha kuweza kuwainua wananchi wake kimaisha, na zaidi ya yote kutoa mchango mkubwa wa kiuchumi. Hili ambalo ni kweli kwa Mtwara ni kweli kwa mikoa mingine kama Kigoma, Manyara, Katavi, Lindi n.k.


Unique Model 2012


Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.

Mwanamitindo wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu.

Washiriki waliongia tano bora.

Washiriki waliongia tano bora.

Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda.

Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani.



Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali.


Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.

Friday, December 28, 2012

ROSE MUHANDO ATIKISA SIKU YA KRISMASI MKOANI IRINGA KATIKA TAMASHA LA MLIPUKO WA LULU ZA INJILI


Mwimbaji Rose Muhando akiwapagawisha wakazi wa Iringa waliofika kushuhudia tamasha hilo uwanja wa samora leo



Baadhi ya wakazi wa Iringa Waliohudhuria katika tamasha hilo





Kwa style hii picha itakayotoka sijui yanikumbusha enzi za analogia

MC wa Tamasha la leo Gerald Malekela



Mgeni rasmi mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa akichangisha fedha kwaajili ya watoto yatima katika mkoa wa Iringa huku na yeye akitoa laki tano katika kusaidia vituo mbalimbali Iringa.

The whispers Band nao walikuwepo kutoa burudani
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Iringa Peter Mgaya akiimba wimbo wa Ndiheledee

SAKATA LA NAIBU WAZIRI WA ELIMU KUWA NA ELIMU FEKI PAMOJA NA JINA FEKI LACHUKUA SURA MPYA.....!



NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, amesema yupo tayari kumthibitishia Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Joseph Mbilinyi, maarufu 'Sugu', juu ya elimu aliyonayo kama alivyodai mbunge huyo.

Bw. Mulugo aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na Majira kuhusu madai ya Bw. Mbilinyi ambayo ameyatoa katika vyombo vya habari kuwa, Waziri huyo ana elimu ya kuunga unga na jina lake kamili ni Amim.

Alisema kauli ya Bw. Mbilinyi haina ukweli wowote bali yeye ni msomi na yupo tayari kuthibitisha ukweli huo kwa umma.

“Mimi na Bw. Mbilinyi tuna vilema vingi, akitaka tuumbuane yatabainika mengi hasa katika upande wake, namfahamu muda mrefu kwa sababu nimesoma naye shule moja, nafahamu mambo yake mengi lakini kutokana na hekima zangu sihitaji malumbano na yeye,” alisema Bw. Mulugo.

Alidai kumshangaa Bw. Mbilinyi, kuzungumzia jambo ambalo halifahamu lakini kwa kumsaidia ili asielendelee kuonekana mwanasiasa muongo, aitishe mkutano na waandishi wa habari na yeye atakuwa tayari kuthibitisha elimu yake kwa umma.

Bw. Mulugo aliongeza kuwa, ni kweli wakati anasoma alikuwa akitumia jina la Amim na baada ya kufika elimu ya juu alianza kutumia jina la Philipo ambalo ni la ukoo ambapo Bw. Mbilinyi kama angekuwa makini, angefuatilia kwenye ukoo wake ili kujua jina hilo linamuhusu au la.

Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo hivi sasa linashikiliwa na Bw. Mbilinyi, mwaka 2015 linarudi CCM na ukweli huo utathibitika katika uchaguzi.

“Mimi ni Waziri kutoka CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu NEC, hivyo Bw. Mbilinyi, asifikiri kuzua maneno hayo yatanitisha hadi nishindwe kutekeleza sera za chama changu,” alisema.

Alisema ibara ya 5 ya Katiba ya CCM, inamwongoza kuhakikisha chama chake kinashinda uchaguzi wa dola wa ngazi zote pamoja na kulirudisha jimbo la Mbeya Mjini kutoka upinzani.

“Katika Uchaguzi Mkuu ujao, nitatumia nguvu zote kuhakikisha jimbo la Mbeya Mjini linarudi CCM, ninachoweza kumshauri Bw. Mbilinyi, ajifunze kutokana na makosa kwani ameanza kunitafuta siku nyingi lakini mimi sikuwa na muda wa kumjibu bali niliendelea kutekeleza majukumu niliyonayo,” alisema.

Alisema Mbunge huyo na chama chake walijibiwa na wananchi wa Saza katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika Wilaya ya Chunya na kusahau kilichowapeleka ni kampeni hatimaye wakaanza kunadi elimu ya Mulugo badala yake waliambulia kufukuzwa.

Aliongeza kuwa, Bw. Mbilinyi alipaswa kulisema na hilo kama walifukuzwa na wananchi wa Saza ambao walimwambia wao, wanamfahamu viziri Bw. Mulugo na wamemsomesha wenyewe kwa pesa zao baada ya kuthibitika ni yatima.

Alisema wananchi hao walidai kuchoshwa na matusi ya Bw. Mbilinyi dhidi yake na kumtungia uongo lakini yeye hana
muda wa kulumbana naye bali atamjibu kwa ushahidi.

Kauli ya Bw. Mulugo imekuja siku chache baada ya Bw. Mbilinyi kudai kuwa, elimu ya Waziri huyo ni ya kuunga unga kwani alisoma naye Sekondari ya Mbeya Day, wakati huo akiitwa Amim si Philipo Mulugo hivyo kuanzia sasa ataendelea kumuita jina lake halisi na kusisitiza hana uwezo wa kumng'oa jimboni kwake. UGOMVI ULIANZIA KWENYE HII HOTU

T.I.D AMFANANISHA ALLY KIBA NA "MTU AMBAYE NI SHOGA"



Khalid Mohamed aka TID mara nyingi amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kueleza hisia zake hasa kuhusiana na muziki.


Leo kupitia Facebook TID amekumbushia lile sakata la kudaiwa kupanga njama za kumuua mwanamuziki mwenzake, Ali Kiba na kumuuita ‘shoga’ yule aliyemzushia hivyo.

“Stupid Thing Ever Happened in Bongo Music Scene is this Homo mentioned me Trying to Kill Him while am only thinkin about this Girl…No Homo,let’s make Hits,” ameandika.

Aliongeza, “Can’t forgive weak people the whole family came into my house as if I ever had any arguments before nau wat……nobody kill them.”

>>>Aliyeitwa shoga ni Ally kiba.....Rejea hii sentensi:-

"Stupid Thing Ever Happened in Bongo Music Scene is this Homo mentioned me Trying to Kill Him "
habari/picha: mpekuzi blog

WASANII DAYNA NA RICH MAVOKO WAWASHUKURU WATANZANIA



Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mwanaisha Nyange a.k.a Dyana akiongea na waandishi wa habari (hawapo) pichani Dec, 28,2012 jijini Dar es Salaam, ametoa shukrani zake kwa Aljazerra Entertaiment kwa kumsaidia kumtoa msanii huyo kimuziki, bila ya kuwasahau, wadau mbalimbali wote wa muziki nchini ambao amesema ndio waliomsaidia kumfikisha hapo alipo sasa katika sanaa hii ya muziki huu wa kizazi kipya, kwani bila ya kupata ushirikiano wao asingeweza kufikia hapa alipo. (kushoto) ni Msemaji wa Aljazerra Entertaiment Simon John.

Msanii Richard Lusinga (a.k.a – Richie Mavoko) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Dec,28,2012 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa shukrani kwa niaba ya Kampuni yake ya Aljazerra Entertaiment, katika shukurani zake amesema,” kama msanii wa kizazi kipya amewaomba radhi kwa wote aliowakosea na yeye pia amewasemehe” Pamoja na Kushukuru kampuni ya Aljazerra Entertaiment, waandishi wa habari na wadau wote wa muziki nchini, kwani ndio waliomfikisha hapo alipofikia na kuahihidi atazidi kuboresha na kuwaletea nyimbo kali zaidi washabiki wake katika mwaka wa 2013. Richie Mavoko anatamba na nyimbo zake kama Mbona silai, Folo folo me, one time na Merry me . (kushoto ) Ni Msanii Mwanaisha Nyange (a.k.a DYANA).

Thursday, December 27, 2012

TIGO YATANGAZA OFA KUPIGA SIMU NNJE YA NCHI.


Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Bulla Bona, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu ofa ya msimu wa sikukuu ya hudumuma ya Xtrime Pack itakayowawezesha wateja kupiga simu kwa gharama nafuu zaidi kwenye nchi 6, UK, USA, Canada, India, Hong Kong or China, dakika 5 kwaTsh 150.

Waandishi wa habari wakiwa kazini kuchukua picha wakati wa kutangaza ofa hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Bulla Bona, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu ofa hiyo, kulia ni Tulli Mwaikenda kutoka Tigo.

Kila kitu ni muhimu kwa picha.

SERIKALI YAAHIDI KUMALIZA TATIZO LA FAO LA KUJITOA


Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (kushoto), akitembelea moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa shule inayotekelezwa na mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara hivi karibuni. Kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.

Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (katikati), akitembelea moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa shule inayotekelezwa na mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.

Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (kulia), akitembelea kituo cha afya cha Nyangoto kilichopo wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara, ambacho kimepata ufadhili mkubwa wa ukarabati na vifaa kutoka kwa mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG). Pembeni ya waziri ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.





SERIKALI imewataka wafanyakazi wa sekta ya madini kuwa watulivu wakati inafanyia kazi malalamiko yao kuhusu fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii, ambapo amesema inaandaa utaratibu maalumu utakaowawezesha wanachama wa mfuko husika kunufaika nao wakiwa kazini ama baada ya kumaliza utumishi wao.


Serikali imewasisitizia wafanyakazi nchini kuwa suala hilo limepewa kipaumbele ili kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.


Ari hiyo ilitolewa hivi karibuni na Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka, wakati akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime, mkoa wa Mara.


Waziri huyo aliwasihi wafanyakazi wenye mawazo ya kuacha kazi ili tu wachukue mafao yao ya kujitoa kuachana na fikra hizo potofu ambazo alisema zitaleta athari kwa familia zao.


Bi.Kabaka amesema serikali imesikia kilio cha wafanyakazi we sekta ya madini na wengine na kwamba kwa pamoja na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wako katika jitihada za kuangalia jinsi ambavyo wanachama walioandikishwa kwenye pensheni kama wanaweza kuanzishiwa utaratibu wa kuweka na kukopa yaani "supplementary scheme."


"Serikali haijafikia uamuzi wakati wowote wa kufanya kuhusiana na mtu ama watu wanaotaka kujitoa katika fao hilo ndio maana niko hapa," alisema.


Alitangaza kuwa serikali itakutana na SSRA na watu wa sekta ya madini jijini Dar es Salaam tarehe 7 Januari, kwa ajili ya kupata mawazo yao juu ya suala la mafao ambapo wafanyakazi wa Migodini watawakilishwa na wawakilishi wao amabo ni chama cha wafanyakazi.


Alisema kuwa serikali haina haraka juu ya suala hilo kwa kuwa inataka kusikiliza mawazo ya wananchama wote, Watanzania, wabunge na wadau mbalimbali ili kupata maoni ambayo yatatafsiriwa kisheria.


Alisema serikali itawasikiliza Watanzania ili kujua ni nini wanapenda kiwepo katika masuala ya hifadhi ya jamii kwa sababu sheria na sera siyo msahafu hivyo inaweza kubadilika kila mara kutokana na mahitaji ya wakati husika.


Waziri Kabaka pia alitembelea miradi mbalimbali ya jamii inayofadhiliwa na mgodi huo wa Barrick na kuisifu kampuni hiyo kwa kusaidia jamii.


Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya na ukarabati mkubwa wa kituo cha afya cha Nyangoto.

MSHINDI WA UNIQUE MODELKUIBUKA LEO


Ile siku iliyosubiriwa na watanzania wengi kutaka kujua nani ataibuka mshindi wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za pekee nchini Tanzania imewadia
Homa ya shindano imezidi kupanda ikiwa usiku wa leo atajulikana nani atavishwa taji la unique model of the year 2012 taji lenye heshima katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania.
Jumla ya washiriki kumi na mbili wanapanda kujwaani kuwania taji hilo ikiwa fainali zake zitafanyika katika ukumbi wa maraha New Maisha club uliopo Oysterbay jijini Dar.
Wanaowania taji hilo ni Vestina Jax,Judith sangu,Amina Ayoub,Catherine Masumbigana,Elizabeth Pertty,Elizabeth Boniface,Vivian Gilbert ,Darline Mmari , Zeenath Habibb,Sandra Suleiman,Cecilia Emmanuel,Magreth Msafiri.
Mratibu wa shindano hili Bwana Methusela Magese amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi siku  wa leo kwani kuna mambo mazuri ya kufurahisha ikiwemo burudani ya muziki wa bendi toka kwa mashujaa,ngoma za asili na bongo flava kwa kiingilio cha Tshs 15,000/= tu.

JAHAZI MODERN TAARAB WAUPAMBA USIKU WA 'BOXING DAY' DAR LIVE


 
MzeeYusuf akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live usiku wa 'Boxing Day'.
Mke wa Mzee Yusuf, Leila Rashid, akizikonga nyoyo za wapenzi wa taarab usiku wa kuamkia leo.
Khadja Yusuf akiwachizisha wapenzi wa taarab ndani ya Dar Live.
Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Fatma Mahmoud 'Mcharuko' akiwapa raha mashabiki.
Nyomi iliyohudhuria shoo hiyo kali kutoka Jahazi Modern Taarab.
Mzee Yusuf akiongea na mashabiki wake.
...Khadja Yusuf kazini.
Bi. Leila Rashid akiendeleza makamuzi.
Mzee Yusuf akizidi kukoleza burudani ndani ya Dar Live.
Wapenzi wa taarab wakijiachia kwa raha zao na Jahazi.
Sehemu ya nyomi iliyotia timu mahali hapo.

---

Kundi la Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake, Mzee Yusuf ' Mfalme' usiku wa 'Boxing Day' lilifanya makamuzi ya nguvu ndani ya ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kuzikonga nyoyo za wapenzi wa taarab waliofurika mahali hapo. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyochukia nafasi wakati wa shoo hiyo.

DIAMOND, DIMPOZ WAFANYA KUFURU USIKU WA X-MAS DAR LIVE

 
...Chezea Diamond wewe!
...Leka dutigite: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Diamond wakiwapagawisha mashabiki kwa wimbo wa Leka dutigite.
Ommy Dimpoz 'on da stage'!
Dimpoz na wasanii wake wakiwasha moto kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki.
...Dimpooo...zzz: Umati ukipiga yowe wakati Ommy Dimpoz akifanya kufuru stejini.
Watu weweee: Kila mmoja akiwa na shauku ya kumpa mkono Diamond.
...Platnumz hewani: Diamond akiwa amebebwa juu na madansa wake.
...Nataka kulewa, zikinipanda nimwage radhi.
 
...Nataka kulewa, lewa...: Diamond akiimba wimbo wake wa Nataka Kulewa.
...Nature ua... Nature ua... Nature ua..: Ndivyo Juma Nature alivyokuwa akienda sambamba kwa staili hiyo na mashabiki.
...Wanaume Halisi wakiendeleza libeneke ndani ya Dar Live.
Mtangazaji wa MTV Base na Choice FM, Vanessa Mdee akichombezana na Ommy Dimpoz wakati wakiimba wimbo wao wa Me & You stejini.
KR Muller akigonga mvinyo ndani ya mask.
...Zitto kazini: Siyo siasa tu, hata mistari mi mkali.
Kikosi cha Diamond Platnumz kazini.
Dimpoz na Vanessa wakipagawisha katika jukwaa la kupanda na kushuka ndani ya Dar Live.
Manjonjo ya madansa wa Dimpoz.
Diamond akiwachizisha mashabiki.
 
Madansa wa Dimpoz wakionyesha umahiri wao.
...Wakizidi kukonga nyoyo za mashabiki.
Zitto Kabwe akicheza kwenye kiti baada ya kunogeshwa na swagga za Dar Live.
 
Platnumz na dansa wake kama 'The Wacko Jacko'.
Shughuli pevu ya Diamond na madansa wake.
...Waacheni watoto waje kwangu: Ndivyo allivyokuwa akichombeza Diamond wakati akitaka kumchukua mtoto huyu.
Platnumz akiipagawisha meza ya wageni waalikwa.
Waalikwa wakionyesha nyuso za tabasamu wakiongozwa na Mwasiti (wa pili kulia) na Prodyuza aliyetengeneza wimbo wa Leka dutigite, Tudi Thomas (wa tatu kushoto).
Prodyuza na Mwanamuziki mkongwe, Ally Mohammed 'Baucha' akikamua stejini.
...Nimpende naniii... Nimpende...: Wapambe "Wemaaaaaaaaaaaaa!"

Madansa wa Extra Bongo wakinogesha zaidi burudani za X-Mas ndani ya Dar Live.

Mpiga gitaa la besi wa Extra Bongo, Hosea Mgoachi akijiachia na shabiki jukwaani.

 

Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa x-mass waliweka historia kwa kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walisindikizwa na mkali Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...